Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta asema bado anasajili

Muktasari:

  • Kocha huyo wa Emirates alisema watafungua milango ya kukaribisha nyota wengine wapya kwenye kipindi hiki cha pre-season wakiwa na ziara huko Singapore huku ikikaribia kabisa kunasa huduma ya straika wa Sporting CP, Viktor Gyokeres kwa ada ya Pauni 63.5 milioni.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amesema kikosi chake bado finyu na hakina viwango vya kutosha hivyo ataendelea kufanya usajili mkubwa kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Kocha huyo wa Emirates alisema watafungua milango ya kukaribisha nyota wengine wapya kwenye kipindi hiki cha pre-season wakiwa na ziara huko Singapore huku ikikaribia kabisa kunasa huduma ya straika wa Sporting CP, Viktor Gyokeres kwa ada ya Pauni 63.5 milioni.

Arsenal imeshafanya usajili wa mastaa wanne kwenye dirisha hili ikitumia zaidi ya Pauni 120 milioni kunasa huduma za wachezaji Martin Zubimendi, Christian Norgaard, Kepa Arrizabalaga na Noni Madueke.

Mastaa watatu kati ya hao wapo na timu hiyo huko Asia, ambapo winga Madueke alihitaji muda wa kumpumzika zaidi baada ya kutoka kwenye fainali za Kombe la Dunia la Klabu kufuatia kukamilisha uhamisho wake wa Pauni 52 milioni kutoka Chelsea.

Arteta anataka kukibadili kikosi chake kuwa bora zaidi, akimsaka Namba 9 wa Sporting, Gyokeres huku pia akiwa na mpango wa kunasa saini ya beki wa Valencia, Cristhian Mosquera kwa ada ya Pauni 16.5 milioni na Arsenal pia ipo kwenye mbio za kumfukuzia winga wa Crystal Palace, Eberechi Eze, anayethaminishwa kwa Pauni 60 milioni.

Kumekuwa na matumaini Gyokeres anaweza kukamilisha usajili wake wa kwenda Arsenal wakati timu hiyo ikijiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya AC Milan huko Singapore, kesho Jumatano.

Arteta alisema: “Tuna kikosi chembamba, tutahitaji kuboresha kuwa kipana. Hivyo bado tutakuwepo sokoni. Bado kuna siku nyingi zimebaki kwenye dirisha hili, lakini hapo dili nyingine zitakapokamilika, tutaendelea kubaki na wachezaji waliopo.”