Arteta ampotezea kabisa Leno

Friday September 17 2021
arteta pic

LONDON, ENGLAND. ISHAKUWA SOO. Mikel Arteta hana uhakika Bernd Leno atakuwa chaguo namba moja katika kikosi chake msimu huu.
Hatma ya Leno bado haijafahamika Arsenal tangu ujio wa Aaron Ramsdale, ambaye ni chaguo la kwanza kwa sasa.
Kipa huyo aliachwa na Arteta kwenye mechi ya Ligi Kuu England wiki iliopita, Arsenal ilipomenyana na Norwich City  ikitoka na ushindiwa bao 1-0.
“Siwezi kumpa ahadi Leno kuhusu uhakika wa namba, muhimu kupambana na kucheza kwa bidii, haiwezi kujitokeza kirahisi,” alisema Arteta.
Leno alianza vibaya msimu akiruhusu mabao mengi katika mechi tatu alizopangwa na Arteta.

Advertisement