Arteta afichua 'kismati' cha Bukayo Saka
Muktasari:
- Winga huyo wa England amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara msimu huu, lakini sasa ameanza kurejea katika kiwango chake bora hasa wakati huu muhimu na Arsenal inaelekea kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza baada ya miaka 20.
LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amesema staa wao Bukayo Saka amekuwa msaada mkubwa hasa kipindi hiki klabu inapambana kushinda mtaji.
Winga huyo wa England amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara msimu huu, lakini sasa ameanza kurejea katika kiwango chake bora hasa wakati huu muhimu na Arsenal inaelekea kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza baada ya miaka 20.
Arteta amesema Saka ni aina ya wachezaji anayebadilisha mechi muda wowote na uwepo wake pekee unaleta hofu kwa timu pinzani.
Ameongeza nyota huyo kwa sasa ana kismati ambacho kinamfanya kuwa mmoja wa wachezaji muhimu zaidi Arsenal na timu ya taifa ya England.
Msimu huu Saka amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya goti, majeraha ya msuli wa nyuma wa paja pamoja na tatizo la Achilles tendinitis, hali iliyomlazimu kukaa nje kwa muda.
Mbali na uwezo wake uwanjani, Arteta amesema mchango wa Saka katika uongozi ndani ya kikosi pia ni mkubwa.
Kocha huyo amefichua mara nyingi humpa Saka unahodha wa timu wakati nahodha mkuu Martin Odegaard hayupo katika kikosi cha kwanza.
Arteta amesema amekuwa akimtegemea Saka kwa sababu ya tabia yake nzuri, moyo wa kujituma na maadili yake ndani ya klabu hiyo.