Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa wanaokwenda Kombe la Dunia la Klabu kibosi

DUNIA Pict

Muktasari:

  • Miamba ya soka ya Ulaya kama Bayern Munich, Real Madrid na Manchester City ni miongoni mwa timu zitakazochuana kwenye michuano hiyo, ambayo itashuhudia mastaa kibao wanaolipwa mishahara mikubwa kwenye klabu zao wakionyeshana ubabe.

NEW YORK, MAREKANI: KIVUMBI cha michuano mipya ya Fifa ya Kombe la Dunia la Klabu kinatarajiwa kuanza Juni 15 hadi Julai 13 na timu 32 zilizopangwa kwenye makundi manane ya timu nne, zitachuana kusaka ubingwa huo huko Marekani.

Miamba ya soka ya Ulaya kama Bayern Munich, Real Madrid na Manchester City ni miongoni mwa timu zitakazochuana kwenye michuano hiyo, ambayo itashuhudia mastaa kibao wanaolipwa mishahara mikubwa kwenye klabu zao wakionyeshana ubabe.

Wakati mashindano hayo ya Fifa yakiwa yamebakiza wiki chache kabla ya kuanza, hii hapa orodha ya wanasoka wanaoongoza kwa kulipwa mishahara mikubwa ambao watakwenda kuonyesha ubabe kuhakikisha timu wanazozitumikia zinaibuka na ushindi.

Kwa mujibu wa Capology, hii hapa orodha ya mastaa 11 wanaolipwa mishahara mikubwa ambao watakuwapo kwenye fainali hizo za Fifa kupigana vikumbo kuwania ubingwa.

DUNI 11

11. Jan Oblak – Pauni 340,625 kwa wiki

Kipa huyo wa Atletico Madrid, Jan Oblak analipwa mkwanja wa maana kuliko makipa makini kabisa kama Ederson, Thibaut Courtois na Gianluigi Donnarumma, ambao wote watachuana kwenye michuano hiyo. Oblak ndiye kipa mwenye mshahara mkubwa zaidi wa wale watakaocheza fainali za Kombe la Dunia la Klabu. Mkataba wake utakwisha 2028 na analipwa Pauni 340,625 kwa wiki.

DUNI 10

10. Vinicius Junior – Pauni 340,625 kwa wiki

Winga wa Kibrazili aliweka mikono yake kwenye FIFA Intercontinental Cup na UEFA Super Cup msimu huu, kinyume na hapo angekuwa na msimu wa ovyo kabisa huko Real Madrid. Lakini, kama atabeba taji la Kombe la Dunia la Klabu, msimu wake unaweza kuwa na afadhali kiasi na akienda kwenye michuano hiyo kama mmoja wa wachezaji wanaolipwa kibosi.

DUNI 09

9. Jude Bellingham – Pauni 340,625 kwa wiki

Kiungo mshambuliaji, Mwingereza, Jude Bellingham analipwa kiwango sawa na mchezaji mwenzake kwenye kikosi cha Real Madrid, Vinicius Junior na wanaweka kibindoni mshahara wa Pauni 340,625 kwa wiki. Jambo hilo linamfanya Bellingham kuwa mchezaji anayeshika namba mbili kwa wakali wa Uingereza wanaolipwa mishahara mikubwa ambao watakuwapo kwenye fainali hizo.

DUNI 08

8. David Alaba – Pauni 367,933 kwa wiki

Alinaswa kama mchezaji huru mwaka 2021, wakala wake beki David Alaba alifanya kazi kubwa kuingia dili za kibabe na Real Madrid ili kumfanya mteja wake kuwa kwenye orodha ya wanasoka wanaolipwa mishahara mikubwa. Kwa wachezaji watakaokuwa kwenye fainali za Kombe la Dunia la Klabu huko Marekani, Alaba, 32, ni miongoni mwa wanaolipwa pochi nene, Pauni 367,933 kwa wiki.

DUNI 07

7. Kevin De Bruyne – Pauni 400,000 kwa wiki

Kiungo wa Kibelgiji, Kevin De Bruyne atakuwa bado ana mkataba kwenye kikosi cha Manchester City wakati michuano hiyo ya Kombe la Dunia la Klabu ikiwa inaanza huko Marekani, licha ya kwamba bado hakuna uhakika kama atakwenda kushiriki. Mkataba wa De Bruyne, 33, utafika tamati Juni 30 na Man City bado haijaweka wazi kama itakwenda na mkali huyo anayelipwa Pauni 400,000 kwa wiki.

DUNI 06

6. Aleksandar Mitrovic – Pauni 408,815 kwa wiki

Fowadi huyo wa Serbia, Aleksandar Mitrovic aliripotiwa alikuwa akilipwa mshahara wa Pauni 80,000 kwa wiki alipokuwa akikipiga katika kikosi cha Fulham, lakini kwa sasa mambo yake yamekuwa matamu, akilipwa kibosi tangu alipojiunga na Al-Hilal ya Saudi Arabia. Katika mechi 76 alizocheza kwenye michuano yote amefunga mabao 65 na mshahara wake ni zaidi ya Pauni 400,000 kwa wiki.

DUNI 05

5. Sergej Milinkovic-Savic – Pauni 408,815 kwa wiki

Kinachovutia mchezaji mwenzake Mitrovic kwenye kikosi cha Al-Hilal, kiungo Sergej Milinkovic-Savic naye analipwa mshahara kama wake wa Pauni 408,815 kwa wiki. Staa huyo mwenye umri wa miaka 30 alijiunga na klabu hiyo ya Saudi Arabia mwaka 2023 na ataweka kibindoni mkwanja unaozidi Pauni 63 milioni endapo kama ataendelea kubaki kwenye timu kwa mkataba wake wote wa miaka mitatu.

DUNI 04

4. Harry Kane – Pauni 408,815 kwa wiki

Straika wa Bayern Munich, Harry Kane analipwa mshahara sawa na wanavyolipwa Mitrovic na Milinkovic-Savic huko kwenye klabu yao ya Al Halal. Lakini, mastaa hao wa soka watakwenda kuonyeshana kazi kwenye fainali za Kombe la Dunia la Klabu huko Marekani ili kuona nani anastahili kulipwa mkwanja mrefu. Mkataba wa Kane unakwisha 2027 na ndiye anayelipwa kibosi Bundesliga.

DUNI 03

3. Kylian Mbappe – Pauni 511,019 kwa wiki

Kama mshambuliaji Kylian Mbappe angeendelea kuichezea Paris Saint-Germain angekuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi kwa wale ambao watakuwapo kwenye fainali za Kombe la Dunia la Klabu huko Marekani. Staa huyo wa Ufaransa alikuwa akilipwa zaidi ya Pauni 1 milioni kwa wiki. Lakini, kwa sasa akiwa kwenye kikosi cha Real Madrid, analipwa Pauni Nusu Milioni kwa wiki.

DUNI 02

2. Erling Haaland – Pauni 525,000 kwa wiki

Baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka tisa na nusu kuendelea kuichezea Manchester City, Januari, straika Erling Haaland amekuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi Ligi Kuu England. Staa huyo naye atakuwapo Marekani akiwa na kikosi cha Man City na hivyo kuwa kwenye orodha ya wanasoka wanaolipwa kibosi ambao watakuwapo kwenye fainali za Kombe la Dunia la Klabu.

DUNI 01

1. Kalidou Koulibaly – Pauni 567,435 kwa wiki

Baada ya kujiunga na Al-Hilal mwaka 2023, Kalidou Koulibaly amekuwa beki anayelipwa mshahara mkubwa zaidi duniani akipokea mkwanja wa Pauni 567,435 kwa wiki. Kutokana na supastaa Cristiano Ronaldo kutokuwapo kwenye fainali hizo baada ya timu yake ya Al-Nassr kushindwa kufuzu, hiyo ina maana, Koulibaly atakuwa mchezaji anayelipwa kibosi zaidi kwenye Kombe la Dunia la Klabu.