Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim ataka beki wa kati Man United

MAN UTD Pict

Muktasari:

  • Akizungumza katika kuelekea mchezo wa fainali ya Europa League utakaopigwa Mei 21, kocha Amorim alitoa tathmini ya mabeki wake majeruhi ambao ni Leny Yoro na Matthijs de Ligt.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim amesema timu hiyo italazimika kuingia sokoni dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi kusajili beki wa kati.

Akizungumza katika kuelekea mchezo wa fainali ya Europa League utakaopigwa Mei 21, kocha Amorim alitoa tathmini ya mabeki wake majeruhi ambao ni Leny Yoro na Matthijs de Ligt.

Yoro alionekana akilia wakati anatolea Old Trafford baada ya kuumia mguu kwenye mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya West Ham. Na beki mwingine wa kati, De Ligt hakucheza mechi yoyote tangu alipoumia dhidi ya Brentford mwanzoni mwa mwezi Mei.

Mabeki wa kati wengine majeruhi kwenye kikosi hicho cha Man United ni Lisandro Martinez na Ayden Heaven na kumfanya Amorim kuwa na machaguo machache ya wachezaji wa nafasi hiyo. Hilo ndilo linalomfanya kocha huyo Mreno kuona kama atahitaji kuongeza beki wa kati mwingine dirisha lijalo.

Alisema: "Leny ni kama Mattha. Nilikuwa nafikiria msimu ujao, kwenye kikosi kama tutataka beki mwingine, kama haya yatakuwa ni majeraha ya muda mtefu. Huo ndiyo wasiwasi wangu, siyo ishu ya fainali tu, japo nahitaji wachezaji wangu wote wawe fiti.

"Yoro ni mguu na amekuwa na tatizo hilo. Ndiyo maana nawaza kuhusu msimu ujao, kikosi kijacho, namna tutakavyoweza kukijenga. Huo ndiyo wasiwasi wangu, wengine watakuwa tayari kwa fainali."

Alipoulizwa wasiwasi wa kuhusu mastaa wengine kama Luke Shaw, Amorim alisema: "Ndiyo, ipo wazi hatuwezi kuwaweka kwenye hatari wachezaji wetu, hasa kwenye nyakati kama hizi."

Baada ya mechi ya Ijumaa usiku dhidi ya Chelsea uwanjani Old Trafford, Man United itakuwa na siku tano za kumpumzika kabla ya kukwaana na Tottenham Hotspur kwenye mchezo wa fainali ya Europa League utakaofanyika huko Bilbao, Hispania, Jumatano ijayo.