Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal yafanya mabadiliko makubwa

ARSENAL Pict

Muktasari:

  • Lewis anaondoka Kaskazini mwa London baada ya kuhudumu kama  mshauri wa kuaminika wa familia ya Stan Kroenke kwa karibu miongo miwili.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL imetangaza mabadiliko makubwa ya uongozi wa klabu huku Tim Lewis, ambaye amekuwa katika klabu kwa muda mrefu, akiaga nafasi yake ya makamu mtendaji.

Lewis anaondoka Kaskazini mwa London baada ya kuhudumu kama  mshauri wa kuaminika wa familia ya Stan Kroenke kwa karibu miongo miwili.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 62 amekuwa akiongoza Kroenke Sports & Entertainment tangu mwaka 2007 na alichaguliwa kuwa mkurugenzi wa Arsenal Septemba 2020.

Lewis alipandishwa cheo kuwa makamu wa kiti cha utendaji Machi 2023. Sasa Richard Garlick atakuwa Mkurugenzi Mtendaji wa klabu, huku Kelly Blaha na Otto Maly wakiwa wamejiunga na bodi kama wataalamu wasio wa utendaji, pamoja na mshauri wa muda mrefu wa KSE, Dave Steiner.

Ben Winston pia ameteuliwa kuwa mkurugenzi lakini sio wa utendaji.

Katika taarifa yake, Josh Kroenke alisema:

“Tuna furaha ya kumteua Rich kuwa Mkurugenzi Mtendaji baada ya kipindi cha mafanikio makubwa akiwa kama Mkurugenzi wa Arsenal. Rich ametoa mchango mkubwa katika nyanja zote huku tukiendelea katika kipindi ambacho tumeendelea kujitahidi kushinda makombe makubwa, kuwa na uchumi imara na kuwapa furaha mashabiki wetu.

“Katika wakati huu, tunapenda kumshukuru Tim kwa kujitolea kwake kwa Arsenal katika kipindi cha mabadiliko makubwa ya klabu. Amekuwa na jukumu muhimu na kuhakikisha tuko katika nafasi nzuri kuendelea kutekeleza mkakati wetu katika azma yetu ya kushinda makombe makubwa.

“Kwa kuzingatia shauku yetu ya kusonga mbele kila wakati, tutaimarisha Bodi yetu kwa kuongeza baadhi ya watu wenye uwezo ambao wataleta uzoefu mkubwa katika nyanja mbalimbali.”

Lewis amekuwa mshauri wa Stan Kroenke tangu mwaka 2007 ambapo alikuwa akianza na uwekezaji wake wa awali katika klabu hiyo.

 Kroenke alinunua hisa ya asilimia 9.9% kutoka ITV plc mwaka 2007. Inaripotiwa kuwa Lewis alijenga uhusiano mzuri na kocha Arteta. Anatajwa alikuwa mtu muhimu katika kumshawishi kocha huyo kusaini mkataba mpya mwaka 2022.

Arsenal imeanza msimu mpya kwa mafanikio licha ya mabadiliko makubwa nyuma ya pazia. Iko nafasi ya pili katika Ligi Kuu baada ya kushinda mechi tatu kati ya nne za mwanzo za ligi.