Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal wawasiliana na wawakilishi wa Frenkie de Jong

TETESI Pict

Muktasari:

  • Benchi la ufundi la Arsenal linamwangalia fundi huyu kama mbadala wa Thomas Partey ambaye ameondoka dirisha hili.

RASMI Arsenal imewasiliana na wawakilishi wa kiungo wa Barcelona, Frenkie de Jong, 28, kwa ajili ya kumsajili katika dirisha hili la majira ya kiangazi.

Benchi la ufundi la Arsenal linamwangalia fundi huyu kama mbadala wa Thomas Partey ambaye ameondoka dirisha hili.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwakani na Barca inahitaji kiasi kisichopungua Euro 70 milioni ili kumuuza dirisha hili na kupunguza shida za masuala ya kifedha zinazowakabili kwa sasa.

Msimu uliopita, de Jong alicheza mechi 46 za michuano yote, akifunga mabao mawili na kutoa asisti mbili.

Licha ya Barca kuonekana kuwa tayari kumuuza haijajulikana ikiwa De Jong  atakuwa tayari kujiunga na washika mitutu hao.

Fundi huyu aliyejiunga na Barcelona mwaka 2019 akitokea Ajax kwa ada ya Euro 89 milioni, pia amecheza jumla ya mechi 70 akiwa na timu ya taifa ya Uholanzi.

Ikiwa atauzwa Barca itakuwa imepunguza eneo kubwa la bili ya mshahara hali itakayowapa nafasi ya kuwaingiza wachezaji wengine katika mfumo kwani staa huyo anakunja takribani Euro 365,385  kwa wiki.


Adam Wharton

MANCHESTER United inaangalia uwezekano wa kuwasilisha ofa Crystal Palace ili kuipata saini ya kiungo wa timu hiyo, Adam Wharton, 21, dirisha hili. Staa huyu alijiunga na Palace  mwaka jana kwa Pauni 22 milioni akitokea Blackburn Rovers na mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029. Man United imemweka fundi huyu katika orodha ya viungo inaowahitaji baada ya kuona huduma ya Baleba imekuwa ngumu kupatikana.


Jadon Sancho

AS ROMA inataka kutoa Pauni 20 milioni ili kumsajili winga wa Manchester United dirisha hili lakini changamoto sasa ni mshahara anaouhitaji ni mkubwa tofauti na kiasi ambacho Roma inaweza kulipa. Sancho ambaye kwa sasa anakunja mshahara wa Pauni 300,000 kwa wiki anaripotiwa kuwaambia Roma kuwa anahitaji Pauni 250,000 kwa wiki jambo ambalo ni gumu kwa timu hyo. Staa huyu alinunuliwa na Man United akitokea Borussia Dortmund.waka 2021 kwa Pauni 73 milioni, mkataba wake unamalizika mwakani.


Tyrell Malacia

MABOSI wa Roma wanazungumza na wawakilishi wa Manchester United ili kuhakikisha wanaipindua Besiktas kumwania beki wa kushoto wa klabu hiyo, Tyrell Malacia mwenye umri wa miaka 26. Malacia, ambaye msimu uliopita alikuwa kwa mkopo PSV, haonekani kuwa katika mipango ya kocha Ruben Amorim ambaye amempa ruhusa ya kutafuta timu nyingine ya kujiunga nayo.


Alessandro Bastoni

INTER Milan imekataa ofa ya Euro 50 milioni kutoka Chelsea inayohitaji saini ya beki wao kisiki  Alessandro Bastoni dirisha hili. Inaelezwa Inter imakataa ofa hiyo kwa sababu Bastoni ni sehemu muhimu ya mpango wa kocha wao Simone Inzaghi msimu huu. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028, Inter itakuwa tayari kumuuza ikiwa itapata ofa kubwa ambayo itawahakikishia kununua mbadala wake.


Xavi Simons

KIUNGO mshambuliaji wa RB Leipzig, Xavi Simons, 22, amewaambia wawakilishi wake na mabosi wa Leipzig timu pekee anayohitaji kujiunga nayo dirisha hili ni Chelsea. Staa huyu ambaye anafuatiliwa kwa karibu na Bayern Munich pamoja na Man City amevutiwa zaidi na mipango ambayo matajiri hao wa Jiji la London wameiwasilisha, hivyo amewachagua wao pekee.


Rasmus Hojlund

AC Milan imewasilisha ofa ya Pauni 30.2 milioni Manchester United kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji  wa klabu hiyo, Rasmus Hojlund, 22, dirisha hili lakini Man United imekataa. Ripoti za ndani zinaeleza mashetani hao wekundu wanahitaji ofa inayoanzia Pauni 40 milioni kumuuza staa huyo aliyejiunga nao mwaka 2023 akitokea Atalanta kwa ada ya Pauni 72 milioni.


Dusan Vlahovic

IKIWA mpango wao wa kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Rasmus Hojlund utafeli, AC Milan wanamwangalia straika wa Juventus, Dusan Vlahovic kama mbadala wake. Mara kadhaa imeripotiwa Juventus ipo tayari kumuuza Vlahovic dirisha hili. Mkataba wa staa huyu unamalizika mwaka 2026 na msimu uliopita alifunga mabao 17 katika mechi 44 alizocheza.