Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal, Manchester City zatabiriwa ubingwa EPL 2025-2026

BINGWA Pict

Muktasari:

  • Smith ambeye aliitumikia The Gunners kuanzia 1987 hadi mwaka 1995, amesema Arsenal na Manchester City ndizo timu pekee zitakazoshindana kwenye mbio za ubingwa, kutokana na kuwa na vikosi imara.

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Alan Smith, ametaja klabu mbili ambazo anaamini zitashindana kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya EPL msimu huu 2025-2026.

Smith ambeye aliitumikia The Gunners kuanzia 1987 hadi mwaka 1995, amesema Arsenal na Manchester City ndizo timu pekee zitakazoshindana kwenye mbio za ubingwa, kutokana na kuwa na vikosi imara.

Gwiji huyo amesema amekuwa mfuatiliaji mzuri wa Ligi Kuu ya EPL msimu huu, na amebaini wazi kuwa Arsenal na Manchester City zina uwezo wa kuendelea kupambana hadi mwisho, hivyo ikitokea mmoja kati yaoa nakuwa bingwa hatoshangaa.

“Ninajua mengi yanazungumzwa katika mbio za ubingwa msimu huu, lakini kwangu niaamini Arsenal na Manchester City zitapambana hadi mwisho na mmoja kati yao atakuwa bingwa msimu huu.

BING 01

“Ninafahamu soka ni mchezo wa ajabu sana, lolote linaweza kutokea na bingwa akawa tofauti na hawa niliowataja, lakini kwa mtazamo wangu na mwenendo unavyokwenda kwa sasa, sina budi kusema Arsenal na Manchester City zinastahili kutajwa kama nilivyofanya mimi.

“Arsenal na Manchester City, itakuwa kama shindano la farasi, ninasubiri ili nione mpambano huu utakavyomalizika mwishoni mwa msimu. Ninaamini utakuwa mzuri sana na wa kusisimua,” amesema Smith

BING 02

Katika kipindi hiki cha karibu miongo miwili, Alan Smith aliunda historia ya Arsenal akiwa mshambuliaji makini na pia akicheza nafasi ya kiungo wa kati wakati mwingine. 

Alijulikana kwa uwezo wake wa kufunga mabao muhimu, mbinu zake za kucheza kwa nguvu na kujituma bila woga kwenye uwanja, jambo lililomfanya kuwa kipenzi cha mashabiki wa Arsenal. 

Akiwa Arsenal, Smith alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu (1988-1989 na 1990-1991), Kombe la Ligi (1993), Ngao ya Jamii (1992) na UEFA Cup Winners' Cup (1993–1994) ambapo katika michuano hiyo, mechi ya fainali alifunga bao pekee dhidi ya Parma, Arsenal ikishinda 1-0. Kwa sasa Smith ni mchambuzi na mtangazaji wa Sky Sports.