Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal, Man City kuanza mbio ubingwa, mechi 10 za mwisho EPL

BUTI Pict

Muktasari:

  • Arsenal inaongoza ligi kwa tofauti ya pointi tano dhidi ya wapinzani wao wa karibu kwenye mbio za ubingwa, Manchester City, ambayo bado ina mchezo mmoja mkononi. Arsenal imepata mzuka wa kukoleza mwendo kwenye mbio za ubingwa baada ya kuichapa Tottenham Hotspur 4-1.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL inaingia kwenye mechi 10 za mwisho za msimu huu ikiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England, lakini inakabiliwa na changamoto ngumu kwelikweli ndani ya miezi michache ijayo kabla ya ligi hiyo kufika tamati.

Arsenal inaongoza ligi kwa tofauti ya pointi tano dhidi ya wapinzani wao wa karibu kwenye mbio za ubingwa, Manchester City, ambayo bado ina mchezo mmoja mkononi. Arsenal imepata mzuka wa kukoleza mwendo kwenye mbio za ubingwa baada ya kuichapa Tottenham Hotspur 4-1.

Hata hivyo, Arsenal ikabiliwa na ratiba yenye msongamano mkubwa kutokana na kufika fainali ya Kombe la Ligi sambamba na kusonga mbele katika Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mashabiki wa Arsenal wanaota ndoto ya kutwaa mataji manne ndani ya msimu mmoja kwa mara ya kwanza katika historia yao baada ya kuwa na msimu mzuri hadi sasa.

Mafanikio yoyote yatakuwa ya kwanza kwao kushinda taji kubwa tangu walinyakua Kombe la FA mwaka 2020. Lakini, wiki za mwisho za msimu zinaweza kuwa za presha kwa Arsenal wanapojaribu kuvuka mstari wa mwisho.

Bado inapaswa kukutana na timu mbili zilizopo kwenye nafasi sita za juu kwa sasa, ikianza na Chelsea uwanjani Emirates wikendi hii.

Arsenal pia itasafiri kukutana na wapinzani wao wa karibu katika mbio za ubingwa, Man City, Aprili, mechi ambayo inaweza kuamua nani atatawazwa bingwa. Chama hilo la kocha Mikel Arteta pia linakabiliwa na dabi nne za London dhidi ya Fulham, West Ham United, Crystal Palace pamoja na Chelsea.

BU 01

Mechi mbili kati ya tatu za mwisho zitakuwa dhidi ya timu zilizo katika eneo la kushuka daraja na zitakuwa zinapambana kusalia Ligi Kuu. Kazi ipo.

Man City inatamani kufuta pengo la pointi tano na inajua itamaliza kileleni ikiwa itashinda mechi zao zote 11 zilizosalia. Kikosi cha kocha Pep Guardiola, kilichoendelea kuweka presha kwa Arsenal baada ya kuifunga Newcastle United, Jumamosi, pia kina ratiba ngumu.

Man City itakutana na timu tatu kati ya sita bora, ambazo ni Chelsea, Arsenal na Aston Villa.

Hata hivyo, mechi mbili kati ya hizo zitachezwa katika Uwanja wa Etihad na ina rekodi bora ya kushinda mechi 11, sare 2 na kupoteza 1, ikiwa ni rekodi bora zaidi katika ligi. Pia ina nafasi nzuri ya kupunguza pengo hilo katika wiki zijazo.

Mechi zao nne zijazo itacheza na Leeds United, Nottingham Forest, West Ham na Crystal Palace, zote zikiwa katika hatari ya kushuka daraja. Aston Villa imesalia nyuma katika mbio za ubingwa na inapaswa kukutana na Chelsea pamoja na Man United mwezi ujao. Pia itakutana na Liverpool kabla ya kusafiri kwenda kukutana na Man City.

Chelsea ina mechi mbili mfululizo za ugenini dhidi ya timu zilizo tatu bora na bado inapaswa kuwakaribisha Man City na Man United katika Uwanja wa Stamford Bridge. Ziara ngumu kwa mabingwa watetezi Liverpool pia iko kwenye ratiba ya kikosi cha Liam Rosenior.

Man United inapanda hadi nne bora baada ya kupata matokeo mazuri dhidi ya Everton usiku wa Jumatatu, shukrani kwa bao la mtokea benchini Benjamin Sesko kwenye kipindi cha pili. Mechi nyingi zilizosalia za Man United zitachezwa Old Trafford.

Liverpool iliimarisha matumaini yao ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi wa dakika za mwisho dhidi ya Nottingham Forest, Jumapili. Mechi zao mbili zijazo itacheza na West Ham na Wolves.

Lakini, mechi tatu kati ya nne zao za mwisho zitawakutanisha Liverpool na wapinzani wakubwa waliopo kwenye sita bora, Man United, Chelsea na Aston Villa. Huu ni mwendo wa kukaza buti.