Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal, Liver, Aston Villa zakomba mamilioni Uefa

Muktasari:

  • Miamba hiyo mitatu ya Ligi Kuu England inashika nafasi ya kwanza, tano na nane mtawalia katika msimamo huo wa timu 36 baada ya mechi za usiku wa Jumanne. Kwa timu zote zilizoshiriki michuano hiyo, kwanza zina uhakika wa kukusanya mkwanja wa Pauni 15,744,700.

LONDON, ENGLAND:

 LIVERPOOL, Arsenal na Aston Villa zinajiandaa kuvuna mkwanja wa maana kwa kumaliza nafasi nane za juu kwenye msimamo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Miamba hiyo mitatu ya Ligi Kuu England inashika nafasi ya kwanza, tano na nane mtawalia katika msimamo huo wa timu 36 baada ya mechi za usiku wa Jumanne. Kwa timu zote zilizoshiriki michuano hiyo, kwanza zina uhakika wa kukusanya mkwanja wa Pauni 15,744,700.

Lakini, kwa mtindo mpya wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, msimu huu mgawo wa ziada kwa maana ya bonasi itatolewa kutokana na nafasi kwenye msimamo.

Bonasi ya jumla itakuwa kwenye mgawo sawa wa hisa zenye thamani ya Pauni 232,516 - kiwango ambacho timu itakayoshika nafasi ya mwisho kwenye msimamo italipwa. Timu itakayoshika nafasi ya 35 timu itapewa hisa mbili, huku mgawo huo ukipangwa kwa nafasi huku timu namba moja itakuwa na hisa 36.

Kwa hadi hapa ilipofika, vinara Liverpool wataweka kibindoni Pauni 8,370,576 kutokana na mgawo wao wa hisa 36.

Timu inayoshika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi, Arsenal yenyewe ambayo itapata mgawo wa hisa 33, itakunja Pauni 6,742,964.

Aston Villa, kwa upande wake itaweka kibindoni Pauni 6,975,480 baada ya kushika nafasi ya saba na mgawo wao utakuwa wa hisa 30.

Kwenye mgawo huo utaongezeka kutokana na pesa ambazo zitapatikana kwenye droo  na kwa kila pot kutakuwa na ongezeko la Pauni 591,675. Timu zitapata ziada ya Pauni 1,775,445 kwa kila ushindi utakaopatikana kwenye hatua ya makundi.

Hiyo ina maana kwa Liverpool baada ya kushinda mechi saba, imeweka kibindoni Pauni 12,428,115.

Arsenal na Aston Villa ambazo kila moja ilishinda mechi nne, zenyewe kila moja imevuna Pauni 7,101,780.

Arsenal ilitarajia kukipiga na Dinamo Zagreb uwanjani Emirates usiku wa jana Jumatano na ushindi utawaongezea mkwanja wao. Aston Villa itasubiri mechi yao ya mwisho dhidi ya mabingwa wa Scotland, Celtic, Jumatano ijayo.