Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal kuingiza Pauni 500,000 kwa kila mechi

ARSENAL Pict

Muktasari:

  • Klabu hiyo ipo kwenye mazungumzo kwa ajili ya kunasa dili tamu na taasisi moja itakayokuwa na kazi ya kugawa chakula na vinywaji kwenye uwanja wake wa Emirates, ambapo inaamini jambo hilo litaiingizia walau Pauni 500,000 kwenye mapato kwa kila mechi.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL imeripotiwa kuwa kwenye mchakato wa kuingia dili litakaloifanya iongeze mapato yake ya kwenye mechi kuanzia msimu ujao.

Klabu hiyo ipo kwenye mazungumzo kwa ajili ya kunasa dili tamu na taasisi moja itakayokuwa na kazi ya kugawa chakula na vinywaji kwenye uwanja wake wa Emirates, ambapo inaamini jambo hilo litaiingizia walau Pauni 500,000 kwenye mapato kwa kila mechi.

Arsenal iliuza mgahawa huo wa chakula kwa taasisi ijulikanayo kwa jina la Delaware North kwenye dili la miaka 20 wakati mara ya kwanza ilipohamia uwanjani Emirates mwaka 2006.

Dili hilo refu linatarajiwa kufika ukingoni wakati wa dirisha la majira ya kiangazi na sasa wameona kitu hicho kinaweza kuiingizia klabu pesa za kutosha itakapofanya dili jingine.

Kipindi hicho klabu ilikuwa inahitaji pesa za kutosha kutokana na kukabiliwa na madeni ya ujenzi wa uwanja. Kuna kipindi Arsenal ilijaribu kutaka kuununua mkataba wake huo na taasisi ya Delaware North ambao wamekuwa wakijinasifu kuwa ni vinara wa ukarimu na huduma bora ya chakula duniani.

ARS 01

Taasisi hiyo ni binafsi inayomiliwa na kampuni ya masuala ya huduma za kijamii duniani. Na kinachoripotiwa ni kwamba Delaware North ni moja ya kampuni nne zinazochuana kunasa dili jipya la kutoa huduma ya chakula na vinywaji kwa mashabiki wa Arsenal wanaokwenda kutazama mechi kwenye Uwanja wa Emirates.

Lakini, dili la sasa litakuwa na mfumo tofauti kabisa ambapo Arsenal imelenga kuingia ubia na kampuni nyingine itakayotoa huduma ya chakula na vinywaji huku ikilenga kupata pesa zaidi.

Katika ripoti ya hesabu za kipesa iliyotolewa Februari, mwaka huu, Arsenal ilitangaza mapato ya Pauni 616.6 milioni.  Kwenye mapato hayo, Pauni 132 milioni zilipatikana kama mapato katika mechi za msimu wa 2023-24, ikilenga kwenye mauzo ya tiketi, vyakula, vinywaji na mambo mengine ikiwamo skafu zinazouzwa wakati wa mechi.

Ripoti ijayo inatarajiwa kuonyesha ongezeko la pesa kutokana na kuongezeka kwa mechi zinazofanyika uwanjani Emirates hasa baada ya klabu hiyo kufika hatua za juu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.

ARS 02

Arsenal ipo pia kwenye mazungumzo ya kuongeza  mkataba wake wa udhamini wa Visit Rwanda. Dili hilo kwa sasa linaiingizia Arsenal Pauni 10 milioni kwa msimu, lakini matazamio ni kwamba pesa itaongezeka kwenye dili jipya lijalo.

Mashabiki wa Arsenal ndoto zao ni kuona Emirates imeboreshwa na kuwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 70,000 hadi 80,000 wanaoketi.

Na mabosi wa klabu hiyo wanafikiria juu ya mpango huo, ambao unaweza kuwafanya kuhamia kwenye Uwanja wa Wembley kwa kipindi cha miaka miwili.

Mashabiki wa Arsenal wanataka kunywa na kupata mlo kwenye eneo kubwa wakiwa pamoja na mashabiki wa imu nyingine tofauti na ilivyo kwa sasa wakiwa wamegawanyishwa kwenye vyumba vidogo.

Jambo hilo linaifanya Arsenal kufikiria kuongeza walau mashabiki 2,000 wakiamini kwamba gharama zake haziwezi kuvuka Pauni 500 milioni na pengine inaweza kuwa Pauni 100 milioni.