Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal imejibu ishu ya Atletico Madrid, yataja wachezaji, viongozi

ARSENAL Pict

Muktasari:

  • Miamba hiyo itakutana baadae leo Jumanne Oktoba 21, 2025 (saa 3 usiku kwa saa za Afrika Mashariki), huku Arsenal ikilenga kuendeleza rekodi yao nzuri baada ya kushinda mechi mbili za awali dhidi ya Athletic Club na Olympiacos.

Arsenal imeomba radhi kwa Atletico Madrid kufuatia klabu hiyo ya Hispania kulalamika ukosefu wa huduma ya maji ya moto, baada ya kufanya mazoezi yao kwenye Uwanja wa Emirates.

Miamba hiyo itakutana baadae leo Jumanne Oktoba 21, 2025 (saa 3 usiku kwa saa za Afrika Mashariki), huku Arsenal ikilenga kuendeleza rekodi yao nzuri baada ya kushinda mechi mbili za awali dhidi ya Athletic Club na Olympiacos.

Katika maandalizi ya pambano hilo, Atletico Madrid ilifanya mazoezi yao ya mwisho jana Jumatatu kwenye Uwanja wa Emirates, lakini timu hiyo ilikumbana na usumbufu kwa kukosa huduma ya kuoga kwa maji ya moto katika vyumba vya vya kubadilishia nguo kutokana na hitilafu ya mifumo ya mabomba.

EMI 01

Atletico ilidai kuwa tatizo hilo liliendelea kwa zaidi ya saa moja, hali iliyowalazimu kurejea hotelini kuoga. Inaripotiwa kuwa Arsenal ilirekebisha tatizo hilo ndani ya dakika 40 baada ya kulifahamu, na maji ya moto yalirejea kabla muda wa mazoezi ya Atletico haujakamilika, lakini kocha Diego Simeone alikuwa tayari amemaliza mazoezi.

Hata hivyo, Arsenal imeomba radhi kwa tukio hilo, ambalo imekiri kusikitishwa kwake huku ikiwaomba radhi, viongozi, wachezaji na maofisa wa Atletico Madrid.

Ingawa UEFA inahitaji kuwepo kwa huduma ya maji ya moto kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwa mujibu wa taratibu za miundombinu ya viwanja, hilo linahusu siku za mechi pekee, siyo mazoezi ya kabla ya mechi.

EMI 02

Arsenal inakwenda kwenye mechi ya leo, ikiwa na kitu cha kujitambia ambapo ilianza vyema kampeni ya michuano ya Ulaya kwa kushinda mechi zote mbili za kundi lao, huku Atletico ikiwa nafasi ya 10 baada ya kushinda mmoja na kupoteza mmoja. 

Timu hiyo ya La Liga ilifungwa bao la dakika za majeruhi kwenye kipigo cha 3-2 dhidi ya Liverpool, lakini ikajibu kwa kishindo kwa kuilaza Eintracht Frankfurt 5-1.