Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal, Barca kasheshe, presha ya ubingwa yapanda

PRESHA Pict

Muktasari:

  • Kwa upande wa Ligi ya Italia zitapigwa mechi nne leo, mecho ya wengi yatakuwa katika mchezo kati ya AC Milan dhidi ya Udinese huku Atalanta ikiwa nyumbani kucheza dhidi ya Juventus.

LONDON, ENGLAND: WASHIKA mitutu wa London, Arsenal wanarejea kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England wakiwa na presha ya ushindi baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo katika michuano ya ndani.

Arsenal ilichapwa dhidi ya Manchester City mabao 2-0 katika fainali ya EFL huku ikiruhusu tena kipigo kingine cha mabao 2-1 katika mechi ya robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Southampton.  

Kocha Mikel Arteta alikiri timu yake ina ‘kazi ya kufanya’ baada ya matokeo hayo, lakini ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Sporting CP kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya umeongeza morali kabla ya kurejea kwenye ligi.

Arsenal ambao wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu England na pointi 70 tofauti ya pointi tisa na City, hawajapoteza katika mechi nane mfululizo za ligi  (Wameshinda 6, Sare2) na wameshinda mechi nne mfululizo. Ukuta wao wameonekana kuwa imara, wakiwa hawajaruhusu bao katika mechi tano kati ya sita na wameshinda mechi saba mfululizo nyumbani kwenye mashindano yote.

Kwa upande mwingine, AFC Bournemouth ambao wapo nafasi ya 13 na pointi 42 wanakuja na rekodi nzuri ya kutofungwa katika ligi kwa mechi 11 mfululizo (Wameshinda 4, Sare 7).

Kocha wao Andoni Iraola ameshuhudia timu yake ikipata ushindi mmoja tu dhidi ya timu zilizo katika nafasi saba za juu, jambo linaloonyesha changamoto kubwa waliyonayo.

Kwa ugenini, Bournemouth hawajawa na matokeo mazuri sana, wakiwa na ushindi mara mbili katika mechi zao 14 za mwisho.

Arsenal walishinda mechi zao nane za kwanza za nyumbani dhidi ya Bournemouth kabla ya kupoteza msimu uliopita.

Bournemouth wamekuwa wakipata matokeo dhidi ya Arsenal katika michezo ya hivi karibuni, wakishinda michezo miwili kati ya mitatu ya mwisho, tofauti na historia ya awali na Arsenal ilikuwa ikitesa dhidi ya timu hiyo.

Mechi nyingine kubwa na nzuri ya kutazama leo ni kati ya Liverpool dhidi ya Fulham. Liverpool ambao wapo nafasi ya tano na pointi 49 wanakabiliwa na kipindi kigumu sana msimu huu huku matokeo yao ya hivi karibuni yakionyesha dalili za hatari ya kumaliza msimu vibaya.

Timu hiyo imepoteza mechi tatu mfululizo katika mashindano tofauti kwa jumla ya mabao 8-1, hali inayoonyesha changamoto kubwa kwa kocha Arne Slot.

Tangu waliporudi kutoka mapumziko ya kimataifa, Liverpool wameruhusu mabao sita bila na pia walikosa hata shuti lililolenga lango katika kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya PSG kwenye michuano ya UEFA.

Licha ya changamoto hizo, Liverpool bado wana rekodi nzuri nyumbani, wakiwa wamepoteza mchezo mmoja kati ya 13 za mwisho za nyumbani (Wameshinda 8, Sare 4, Kupoteza 1).

Kwa upande mwingine, Fulham wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na matumaini makubwa baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Burnley. Wamepoteza mechi moja kati ya tano za ligi za mwisho (Wameshinda 3, Sare 1).

Hata hivyo, changamoto kubwa kwa Fulham ni michezo ya ugenini, kwani wameshinda mechi nne za ligi (Sare 3, Kupoteza 8), ingawa hawajapoteza katika mechi zao mbili za mwisho ugenini (Wameshinda 1, Sare 1).

Kwa upande wa Ligi ya Ujerumani wakati Dortmund ikiwa nyumbani kucheza dhidi ya Bayer Leverkusen, FC Bayern Munich wanaendelea na safari yao ya kusaka ubingwa wa 35 wa Bundesliga kwa kucheza dhidi ya FC St. Pauli ambayo inapigania kuwa mbali na hatari ya kushuka daraja.

Huko Hispania kwenye La Liga, FC Barcelona wanakabiliwa na hatari ya kupoteza dabi mbili za Catalonia katika msimu mmoja dhidi ya wapinzani tofauti kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 1966/67.

Hii ni kutokana na RCD Espanyol kwenda Camp Nou wakiwa na nia ya kumaliza ukame wao mrefu wa kutoshinda mechi ya ligi dhidi ya Barcelona.

Barcelona walikumbana na kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Atletico Madrid Jumatano katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya UEFA, matokeo yaliyotibia rekodi ya uya kucheza mechi tisa bila kupoteza (Wameshinda 8, Sare 1).

Hata hivyo, mambo yako tofauti kwenye La Liga, ambapo Barcelona wanaongoza ligi wakiwa na tofauti ya pointi saba kabla ya mechi hii. Hii inawapa nafasi nzuri sana ya kutwaa ubingwa huku ushindi wao wa mechi zote 15 za ligi nyumbani msimu huu ukionyesha ubabe wao nyumbani.

Kwa upande wa Ligi ya Italia zitapigwa mechi nne leo, mecho ya wengi yatakuwa katika mchezo kati ya AC Milan dhidi ya Udinese huku Atalanta ikiwa nyumbani kucheza dhidi ya Juventus.