Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal bado moja tu kutoboa UEFA, Jesus arejea baada ya siku 342

Muktasari:

  • Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta alifanya mabadiliko matano kwenye kikosi kilichopoteza dhidi ya Aston Villa Jumamosi iliyopita, na mmoja wa wachezaji aliowapumzisha siku hiyo, Noni Madueke ndiye aliyeanza kuionyesha thamani yake kwa kufunga bao la kwanza katika mechi hiyo iliyochezwa usiku wa Desemba 10, 2025 kwenye Uwanja wa Jan Breydel, Ubelgiji.

BRUGES, UBELGIJI: Noni Madueke amefunga mabao mawili wakati Arsenal ikiibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Club Brugge na kuendeleza rekodi yao ya asilimia 100 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, hatua ambayo imeiweka timu hiyo atua chache zaidi kufuzu 16 bora bila kupitia mchujo.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta alifanya mabadiliko matano kwenye kikosi kilichopoteza dhidi ya Aston Villa Jumamosi iliyopita, na mmoja wa wachezaji aliowapumzisha siku hiyo, Noni Madueke ndiye aliyeanza kuionyesha thamani yake kwa kufunga bao la kwanza katika mechi hiyo iliyochezwa usiku wa Desemba 10, 2025 kwenye Uwanja wa Jan Breydel, Ubelgiji.

Winga huyo wa England aliwazidi nguvu mabeki wa Club Brugge, akapiga shuti kali kutoka yadi 20 lililogonga mwamba wa juu kabla ya kutinga wavuni.

Club Brugge ilijitahidi kutishia safu ya ulinzi ya Arsenal iliyofanyiwa mabadiliko muda mfupi kabla ya mapumziko, lakini kipa David Raya aliokoa kwa ustadi mashuti ya Christos Tzolis na Aleksandar Stankovic, akaiweka Arsenal kwenye usalama.

Madueke alipachika bao lake la pili dakika mbili tu baada ya kipindi cha pili kuanza, alipounganisha kwa kichwa krosi murua ya Martin Zubimendi. Gabriel Martinelli naye alihakikisha ushindi huo kwa kupiga shuti la kupinda safi dakika ya 56 na kuifanya Arsenal kuhitimisha mabao matatu.

Kulikuwa na habari njema zaidi kwa Arsenal, kwani Gabriel Jesus alicheza kwa mara ya kwanza zikipita siku 342 baada ya kupona majeraha ya kupasuka kwa kano ya goti (ACL), na kijana mwenye umri wa miaka 16, Marli Salmon, akipata nafasi ya kucheza kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha kwanza.

Jesus karibu arejee na bao baada ya kupiga shuti kali dakika za mwisho, lakini mpira ukagonga mwamba.

Ushindi huo umeifanya Arsenal kufikisha pointi 18, ikihitaji moja pekee katika mechi mbili zilizobaki dhidi ya Inter Milan na Kairat ili kumaliza nafasi nane za juu na kufuzu moja kwa moja 16 bora.

Hiyo itaifanya Arsenal kukwepa mechi za mchujo mwezi Februari 2026 na kujiandaa moja kwa moja kucheza hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

Kwa sasa Arsenal yenye pointi 18 ikiongoza msimamo wa Ligi ya Mabingwa, timu ambazo zinaweza kukaa juu yake ikitokea imepata pointi moja pekee katika mechi mbili zilizobaki, ni zile zilizopo nafasi tano za juu, hivyo itakuwa na uwezo wa kumaliza nane bora.

Ikumbukwe kuwa, Ligi hiyo yenye timu 36, baada ya kumaliza hatua hii ya kwanza, zile nane za juu zitavuka moja kwa moja kucheza 16 bora, huku zitakazoshika nafasi kuanzia ya tisa hadi 24 zikicheza mtoano nyumbani na ugenini kupata timu zingine nane kuungana na zile za juu kuedelea na michuano.

Kuanzia nafasi ya 25 hadi 36, zitakuwa zimetolewa moja kwa moja.