Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Antony, Man United basi tena, Atletico yatia neno

Muktasari:

  • Manchester United inadaiwa ni kama imeshamalizana na Antony na ipo tayari kumtoa tena kwa mkopo, licha ya kuonyesha ubora katika LaLiga ambako hadi sasa amehusika na mabao 11.

WWINGA wa Manchester United na timu ya taifa ya Brazil, Antony Matheus dos Santos maarufu kama Antony, 25, hana nafasi ya kurudishwa msimu ujao baada ya mkopo wake Real Betis kumalizika mwisho wa msimu huu.

Manchester United inadaiwa ni kama imeshamalizana na Antony na ipo tayari kumtoa tena kwa mkopo, licha ya kuonyesha ubora katika LaLiga ambako hadi sasa amehusika na mabao 11.

Hata hivyo, kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone amemtaja Antony kuwa mshambuliaji mwenza bora kwa Julian Álvarez.   

Mchezaji huyo amezivutia timu nyingi kumsajili kwa ajili ya msimu ujao, lakini hofu kubwa ni kuhusu mshahara wake wa Pauni 200,000 ambao ni mkubwa na inaelezwa hataki kuupuguza.

Mkataba wa sasa wa Antony na Machester United unatarajiwa kumalizika baada ya mwisho wa msimu ujao.


Ronald Araujo

RONALD Araujo, 26, anaweza kuwa usajili wa sita ghali zaidi katika historia ya Manchester United endapo itakamilisha ofa ya Pauni 67.9 milioni kwa beki huyo wa kati wa Barcelona. Araujo tangu dirisha lililopita la usajili wa majira ya kiangazi alidaiwa kuwa huenda akauzwa kama mkakati wa Barca kufukia mashimo katika vitabu vya fedha. Mkataba unaisha 2029.


Rodrygo

MANCHESTER City inapambana kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Rodrygo Goes, 24, kwa ajili ya msimu ujao na inaelezwa tayari imeshawasilisha ofa tatu. Hata hivyo, Madrid haipo tayari kumruhusu nyota huyo wa Kibrazili kuondoka isipokuwa kama yeye mwenyewe ataomba kuondoka. Mkataba wake unamalizika majira kiangazi 2028.


Brahim Diaz

MMSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Morocco na Real Madrid, Brahim Diaz, 25, ameingia katika 18 za Arsenal kuelekea dirisha lijalo la usajili wa majira ya kiangazi, baada ya timu hiyo kujitoa kuwania saini ya mchezaji mwenzake, Rodrygo. Kinachoelezwa kwa sasa ni kuwa Diaz ambaye hana uhakika wa namba Madrid anazifikiria ofa nyingi mezani. Mkataba wake unamalizika 2027.


Marcus Rashford

STRAIKA wa Machester United na England, Marcus Rashford, 27, anayecheza kwa mkopo Aston Villa amepewa taarifa kwamba Villa inaweza kumsajili moja kwa moja kwa Pauni 40 milioni endapo itafuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Rashford na timu yake wanajadali ofa mbalimbali walizonazo ikiwamo ya PSG na Barcelona. Mkataba wa sasa unamalizika 2028.


Miguel Gutierrez

ATLETICO Madrid na Real Madrid zinapimana ubavu katika vita ya kuwania saini ya beki wa kushoto wa Girona na Hispania, Miguel Gutierrez, 23, kwa ajili ya dirisha lijalo la majira ya kiangazi, huku kila moja ikidaiwa kumhakikishia kuwa ikimsajili atakuwa na uhakika wa namna kikosini. Gutierrez anayemaliza mkataba 2027 msimu huu amecheza mechi zote isipokuwa mbili za mashindano yote.


Jeremie Frimpong

BARCELONA imeanza kuinyatia saini ya beki wa Bayer Leverkusen na Uholanzi, Jeremie Frimpong, 25, huku pia ikimuweka kwenye rada Domilson Cordeiro dos Santos ‘Dodo’ wa Fiorentina na Vanderson de Oliveira Campos wa Monaco iwapo itashindwa kumpata Frimpong. Frimpong pia yupo kwenye rada za Liverpool kama mbadala wa Trent Alexander-Arnold.


Yangel Herrera

KIUNGO wa kati wa Girona na Venezuela, Yangel Herrera, 27, amezivutia Nottingham Forest, Newcastle United na Atletico Madrid kwa dirisha lijalo la usajili wa majira ya kiangazi kutokana kiwango bora anachoendelea kukionyesha, ambapo tangu msimu huu ulipoanza amecheza mechi 26 na kufunga mabao manne huku akitoa asisti tatu.