Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Antoine Griezmann kuondoka Atletico Madrid

ANTON Pict

Muktasari:

  • Kupitia ukurasa wa X wa Fabrizio Romano, Orlando City imepiga hatua kubwa katika mazungumzo hayo, huku ikiwa na matarajio makubwa ya kumsajili mshambuliaji huyo kutoka Ufaransa.

MSHAMBULIAJI nyota wa Atlético Madrid, Antoine Griezmann, anatarajiwa kuachana na klabu hiyo ya Hispania, akihusishwa kuhamia Orlando City ya Marekani ambayo inaendelea na mazungumzo ya kumsajili katika kipindi hiki.

Kupitia ukurasa wa X wa Fabrizio Romano, Orlando City imepiga hatua kubwa katika mazungumzo hayo, huku ikiwa na matarajio makubwa ya kumsajili mshambuliaji huyo kutoka Ufaransa.

“Orlando City imepiga hatua kubwa katika mazungumzo ya kumsajili Antoine Griezmann kutoka Atlético Madrid.” ameandika Fabrizio Romano.

Orlando inataka kukamilisha dili hilo la Griezmann, ikiwa ni wiki chache baada ya mkurugenzi wa klabu hiyo Ricardo Moreira kufanya ziara jijini Madrid, Hispania.

Kuondoka kwa Griezmann, kunachangiwa na usajili wa mshambuliaji wa Nigeria Ademola Lookman akitokea Atalanta ya Italia. Inaonekana klabu hiyo ya LaLiga iko tayari kumruhusu Mfaransa huyo kuondoka, hasa baada ya Lookman kuonyesha kiwango kizuri katika mwanzo wa maisha yake Hispania, akifunga mabao manne na kutoa pasi mbili za mabao tangu atue Januari 2026.

Hali hii inatoa ishara kwamba Atletico Madrid inazingatia kubadilisha safu yake ya ushambuliaji huku wachezaji wapya wakianzia nafasi za kimfumo, huku Griezmann akitarajiwa kuanza safari mpya katika Ligi Kuu Marekami (Major League Soccer).

Antoine Griezmann alisajiliwa Atlético Madrid Julai 2014, akitokea Real Sociedad akicheza kwa miaka tisa katika klabu hiyo, ingawa alihamia FC Barcelona kwa kipindi kifupi kati ya 2019 na 2021. 

Katika kipindi chake akiwa Atlético Madrid, Griezmann ameibuka kuwa mshambuliaji muhimu na kiongozi wa kikosi, akichangia kwa kiasi kikubwa kwenye matokeo muhimu.

Miongoni mwa mafanikio yake, Griezmann alisaidia Atletico Madrid kushinda UEFA Europa League 2017–18, akiwa mchezaji muhimu katika kikosi. Pia alishirikiana katika ushindi wa UEFA Super Cup 2018 dhidi ya Real Madrid. 

Katika ligi ya Hispania (LaLiga), amefunga mabao mabao 133 kabla ya kuhamia Barcelona, na kuendelea kuonyesha ujuzi wake wa kipekee wa ushambuliaji na kutoa pasi za mabao muhimu.

Mbali na mafanikio ya klabu, Griezmann pia alichangia kwa kiasi kikubwa katika timu ya taifa ya Ufaransa akiwa sehemu ya kikosi kilichotwaa ubingwa wa Kombe la Dunia 2018, jambo lililoimarisha hadhi yake ya kimataifa. 

Ana sifa ya mchezaji mwenye mbinu za kufunga, kasi ya juu, na uwezo wa kuongoza kikosi, jambo lililomfanya kuwa sehemu ya muhimu ya Atlético Madrid katika mashindano ya ndani na ya Ulaya.