Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Antony aangua kilio kisa kukosa bao

ANTONY Pict

Muktasari:

  • Betis ilitoka sare ya bao 1-1 na Rayo, Jumamosi katika Uwanja wa Estadio de La Cartuja na kushindwa kupunguza pengo dhidi ya Atletico Madrid, walioko nafasi ya nne, ambayo kwa sasa iko mbele kwa pointi sita katika nafasi za kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.

MADRID, HISPANIA: WINGA wa Kibrazili, Antony hakuwa na namna nyingine zaidi ya kumwaga tu machozi baada ya kushindwa kufunga bao la ushindi kwa Real Betis dhidi ya Rayo Vallecano inayopambana kukwepa kushuka daraja.

Betis ilitoka sare ya bao 1-1 na Rayo, Jumamosi katika Uwanja wa Estadio de La Cartuja na kushindwa kupunguza pengo dhidi ya Atletico Madrid, walioko nafasi ya nne, ambayo kwa sasa iko mbele kwa pointi sita katika nafasi za kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Antony alishindwa kumfunga kipa wa Rayo, Augusto Batalla, katika nafasi ya moja kwa moja wakati wa dakika za majeruhi.

Cedric Bakambu aliwafungia wenyeji bao la kuongoza dakika ya 16, lakini Rayo ambayo iko pointi mbili tu juu ya mstari wa kushuka daraja huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi, walisawazisha kupitia kwa Isi Palazon dakika tatu kabla ya mapumziko.

Hata hivyo, Betis ilikaribia kupata bao katika dakika ya nne ya muda wa nyongeza wakati Antony alipojikuta uso kwa uso na Batalla.

Cucho Hernandez alimwachia mpira winga huyo ndani ya eneo la hatari na mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United alihitaji tu kumpita kipa huyo. Lakini, mchezaji staa huyo kimataifa wa Brazil alipiga mpira moja kwa moja mikononi mwa kipa huyo wa Argentina, hali iliyosababisha mshangao mkubwa miongoni mwa mashabiki uwanjani hapo.

Baada ya filimbi ya mwisho, kamera zilimlenga Antony ambaye alishindwa kujizuia na kuanza kulia. Mbrazili huyo alivunjika moyo kiasi kwamba wachezaji wenzake wa Betis pamoja na mkurugenzi wa michezo, Manu Fajardo walilazimika kumbembeleza na kumfariji ili anyamaze.

Kwa mujibu wa kipindi cha michezo cha El Chiringuito, nyota huyo wa zamani wa Ajax alivunjika moyo sana kutokana na nafasi kubwa aliyokosa katika dakika za mwisho za mechi hiyo ya ligi. Antony amekuwa na Betis tangu Januari 2025 alipohamia Hispania kwa mkopo kutoka Man United, ambako hakuwahi kung’ara, ambako alifunga mabao 12 tu na asisti tano katika mechi 96.

Lakini, Antony alifanikiwa kufufua kiwango chake katika nusu ya pili ya msimu uliopita akiwa Betis, ambao walivutiwa sana hadi wakaamua kumnunua jumla kwa Pauni 21.5 milioni wakati majira ya joto yaliyopita.