Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Anthony Gordon, Ndiaye watajwa Liverpool

Hashim Lundenga aliyekuwa anasimamia mashindano ya Miss Tanzania tangu mwaka 1994 hadi 2018

Muktasari:

  • Mara kadhaa imewahi kuripotiwa, Newcastle inahitaji takribani Pauni 90 milioni ili kumwachia Gordon ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2030.

LIVERPOOL inataka kuimarisha safu yake ya ushambuliaji msimu ujao na inawaangalia mastaa wawili ambao ni winga wa Newcastle United na England, Anthony Gordon, 25, pamoja na mshambuliaji wa Everton na Senegal, Iliman Ndiaye, 26.

Hata hivyo, kuipata saini ya Gordon inaonekana kuwa kazi ngumu kutokana na kiasi kikubwa cha pesa ambacho Newcastle inakihitaji ili kumuuza.

Mara kadhaa imewahi kuripotiwa, Newcastle inahitaji takribani Pauni 90 milioni ili kumwachia Gordon ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2030.

Kuna uwezekano mkubwa Liverpool ikawasilisha ofa ya kwanza inayoweza kufikia Pauni 60 milioni.

Kwa upande wa Ndiaye, mchezaji mwenyewe ameonyesha kuwa yupo tayari kuhamia kwa mahasimu hao wa Everton lakini changamoto kubwa ipo kwa mabosi wa klabu yake ambao hawataki kumuuza kwenda kwa majogoo hao ambao ni wapinzani wao wa karibu.

Inaelezwa kwamba, Everton inaweza kuweka bei kubwa ili kuifanya Liverpool ishindwe kufanikisha mchakato wa kumsajili staa huyo.


Gabriel Jesus

ARSENAL inaripotiwa kuwa tayari kumuuza mshambuliaji wao wa kimataifa wa Brazil Gabriel Jesus, 29, pamoja na kiungo raia wa Ujerumani Kai Havertz, 26, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ili kupata fedha za kusajili mshambuliaji wa Atlético Madrid, Julian Alvarez, 26.

Álvarez amekuwa mmoja ya  mastaa wanaowindwa sana na Arsenal tangu mwaka jana. Kocha Mikel Arteta amevutiwa sana na kiwango cha fundi huyu ambaye kwa sasa anashika nafasi ya nne katika orodha ya wafungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, akiwa ameingia kambani mara tisa.


Marcos Senesi

TAARIFA zinaeleza Liverpool inaongoza katika mbio za kuwania saini ya beki wa Bournemouth na timu ya taifa ya Argentina, Marcos Senesi, 28, ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu.

Kupatikana bure kwa  Senesi mwisho wa msimu huu, kunaonekana kuzivutia timu nyingi England zinazohitaji kuboresha safu zao za ulinzi.

Tangu kuanza kwa msimu huu, Senesi amecheza mechi 33 za michuano yote na kutoa asisti nne.


 

Givairo Read

MANCHESTER City inaendelea kumfuatilia kwa karibu beki wa pembeni wa Feyenoord, Givairo Read, 19, kuelekea dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Mbali ya Man City, Bayern Munich pia imeonyesha nia ya kumsajili nyota huyo chipukizi, jambo linaloongeza ushindani wa kuiwania  saini yake.

Read anatajwa kuwa mmoja wa mabeki vijana wanaokuja kwa kasi. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.


Karim Coulibaly

CHELSEA na Newcastle United ni miongoni mwa timu zinazodaiwa kuwa katika vita ya kuiwania saini ya  beki kinda  wa SV Werder Bremen, Karim Coulibaly, 18.

Coulibaly ameibuka na kuvutia sana vigogo barani Ulaya baada ya kufanya vizuri msimu huu  ambao ni wa kwanza kwake katika Bundesliga.

Ripoti zinadai mabosi wa Bremen wapo tayari kumuuza staa huyu lakini kwa bei mbaya inayoanzia Pauni 60 milioni.


Alisson Becker

JUVENTUS inaendelea kufuatilia kwa karibu hali ya kipa wa Liverpool Alisson Becker, 33, pamoja na kiungo wa Manchester City, Bernardo Silva, 31, kuelekea dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Juventus inapanga kufanya mabadiliko makubwa ya kikosi, ikilenga kusajili mastaa wenye uzoefu wa michuano mbalimbali.

Alisson anadaiwa kutaka kutafuta changamoto mpya sehemu nyingine na anaweza kuuzwa kwa kiasi kisichozidi Pauni 30 milioni.


Ousmane Diomande

NEWCASTLE United ipo tayari kurejea tena na ofa mpya kwa beki wa kati wa Sporting Lisbon, Ousmane Diomande, 22, inayehitaji kumsajili katika dirisha la majira ya kiangazi.

Newcastle ilionyesha nia ya kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast tangu dirisha la Januari, lakini ilishindwa kufikia makubaliano kutokana na msimamo mkali wa Sporting katika masuala ya ada ya uhamisho.

Inaelezwa Sporting hawako tayari kumuachia Diomande kwa dau chini ya Pauni 40 milioni, jambo lililowashinda Newcastle kwa wakati huo.


Jacobo Ramon

BEKI wa kati wa Como 1907 ya Italia, Jacobo Ramon, 21, yupo katika rada za  klabu kadhaa kubwa Ulaya, ikiwemo Arsenal na Chelsea kuelekea dirisha la majira ya kiangazi.

Ramón anatajwa anatazamwa na maskauti wa timu nyingi tangu kuanza kwa msimu huu hali inayoongeza ushindani wa kuwania saini yake kwa sababu wengi wameonekana kuvutiwa na maendeleo yake. Mkataba wa sasa wa Ramon unatarajiwa kumalizika mwaka 2030. Msimu huu amecheza mechi 31 za michuano yote.