Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Anderson kusababisha Manchester derby

ANDERSON Pict

Muktasari:

  • Majirani hao wote wawili wamemweka nyota huyo wa England na Nottingham Forest kama mmoja wa malengo yao makuu katika usajili wa dirisha lijalo ili kuimarisha vikosi vyao kwenye eneo la katikati ya uwanja.

MANCHESTER, ENGLAND: MAHASIMU wakubwa England, Manchester United na Manchester City wanatarajiwa kukabiliana katika vita ya kumsajili kiungo Elliot Anderson dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Majirani hao wote wawili wamemweka nyota huyo wa England na Nottingham Forest kama mmoja wa malengo yao makuu katika usajili wa dirisha lijalo ili kuimarisha vikosi vyao kwenye eneo la katikati ya uwanja.

Anderson ameibuka kuwa mmoja wa viungo bora barani Ulaya tangu alipojiunga na Forest akitokea Newcastle United kwa ada ya Pauni 35 milioni mwaka 2024. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amejiimarisha katika kikosi cha taifa cha England na atakuwa sehemu ya mipango ya Kombe la Dunia ya kocha Thomas Tuchel baadaye mwaka huu.

Man United na Man City zote zinataka kuimarisha safu yao ya kiungo msimu huu wa joto na zinatarajiwa kuingia kwenye vita ya kusaka huduma ya nyota huyo anayekadiriwa kuwa na thamani ya Pauni 75 milioni. Hata hivyo, huku Kombe la Dunia likitarajiwa kuanza mwezi Juni, bado haijulikani kama klabu yoyote itaweza kukamilisha dili hilo kabla ya mashindano hayo. Anderson angependa mustakabali wake ujulikane kabla ya kuelekea kwenye mashindano hayo.

Lakini, anafahamu kuwa thamani yake itapanda zaidi iwapo ataweza kusaidia England kufanya vizuri katika michuano itakayofanyika Amerika Kaskazini. Anderson pia anatambua kuwa anaweza kushuka daraja akiwa na Forest msimu huu.

Hata hivyo, lolote litakalotokea, atakuwa na fursa ya kuchagua kati ya klabu kubwa na anaamini yuko tayari kupiga hatua kwenda kiwango cha juu zaidi. Man United italazimika kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya ili kuwa na nafasi ya kuishinda Man City katika kinyang’anyiro cha kupata saini ya Anderson. Forest haitakuwa na chaguo ila kumuuza Anderson iwapo itashuka daraja na kurejea Championship.