Amrabat aingia anga za Juve, Milan

AC Milan na Juventus zinaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Fiorentina na Morocco, Sofyan Amrabat ambaye kwa sasa anaichezea Manchester United kwa mkopo.
Hadi sasa Man United haijaonyesha nia ya kutaka kumsainisha mkataba wa kudumu Amrabat aliyejiunga nao katika dirisha lililopita la majira ya baridi.

Amrabat alijiunga na Man United kwa mkopo uliokuwa na ada ya Euro 9 milioni na kuna kipengele cha kumnunua mazima kwa Euro 25 milioni.

Juventus ndio imeripotiwa kuwa ya kwanza kutaka kumsajili staa huyu lakini Milan nayo imeibuka katika siku za hivi karibuni na ndio inaonekana kuwekeza nguvu kubwa zaidi.

Milan inataka kumsajili Amrabat kwa sababu inapitia changamoto eneo lao la kiungo hususani katika upande wa kuzuia.

Amrabat alitua Man United baada ya mashetani hao wekundu kushinda vita dhidi ya Barcelona.

Tangua atue kiungo huyu amecheza mechi 22 za michuano yote. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2025.