Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim, Rashford vita bado mbichi

Muktasari:

  • Kocha huyo amesema staa huyo lazima abadilike ili kurudi kikosini na tofauti na hapo hatorudishwa kikosini.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim amefunguka tena kuhusu maendeleo ya mshambuliaji wa timu hiyo, Marcus Rashford na uwezekano wa kurudishwa kikosi cha kwanza.

Kocha huyo amesema staa huyo lazima abadilike ili kurudi kikosini na tofauti na hapo hatorudishwa kikosini.

Amorim alisisitiza kumweka nje mshambuliaji huyo sio kwa sababu zake binafsi, bali inatokana na utendaji kazi na  haijalishi nini kitatokea, hatobadili msimamo wake.

Rashford, ambaye anatamani kuhamia Barcelona baada ya kusema anataka “changamoto mpya,” hajacheza mechi 11 na amekuwa hajumuishwi hata kwenye safari za timu kabisa.

Hivi karibuni, Amorim alisema angemchagua kocha wake wa makipa mwenye umri wa miaka 63, Jorge Vital, badala ya kumchezesha mchezaji yeyote ambaye hafanyi kile ambacho anahitaji.

Kocha huyo Mreno mwenye msimamo mkali amesema Rashford hajawa akifanya mazoezi kwa kiwango cha kutosha ili kujumuishwa katika kikosi na amesisitiza hali hiyo haitabadilika hadi atakapobadilika.

"Tazama timu yetu na ulinganishe na sifa za wachezaji waliopo. Fikiria mchezaji mwenye kipaji kama Rashford, timu yetu ingekuwa bora zaidi, lakini lazima abadilike. Iwapo atabadilika tutamtumia, lakini kwa sasa inapaswa kuwa hivyo kwa sababu hajafika tunakohitaji. Tunasubiri kuona kama Marcus kweli anataka kubadilika. Sina chochote dhidi ya Marcus ikiwemo chuki binafsi dhidi yake," alisema Amorim.

Kocha huyu pia alitoa ufafanuzi juu ya kauli yake ya kusema yupo tayari kumchezesha kocha wa makipa badala ya mchezaji asiyejituma jambo lililoonekana kumlenga Rashford kwa asilimia nyingi.

"Kauli yangu ilikuwa kuhusu kila mchezaji ambaye haonyeshi kiwango chake cha juu kabisa. Sikusema ni kuhusu Marcus pekee. Nitakapohisi ni wakati sahihi, nitampa nafasi yoyote mchezaji yeyote kucheza.

Sisi ni timu bora zaidi tukiwa na Marcus Rashford, lakini sitobadili mawazo yangu hadi pale atakapobadilika. Nimeshazungumza kuhusu Marcus. Chochote nitakachosema kitakuwa mjadala."