Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim ataka kumrudisha Sancho, Garnacho

GYOKERES

Muktasari:

  • Alejandro Garnacho, Jadon Sancho, Antony na Tyrell Malacia ni miongoni mwa mastaa ambao wamepewa taarifa kwamba watafute timu mpya za kujiunga nazo na kwa sasa wanafanya mazoezi Carrington wakati wachezaji wenzao wakiendelea na maandalizi ya msimu mpya huko Marekani.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim amethibitisha kuwa yuko tayari kuwarudisha wachezaji waliopewa ruhusa ya kuondoka katika dirisha ikiwa itashindikana kuuzwa katika dirisha hili la majira ya kiangazi.

Alejandro Garnacho, Jadon Sancho, Antony na Tyrell Malacia ni miongoni mwa mastaa ambao wamepewa taarifa kwamba watafute timu mpya za kujiunga nazo na kwa sasa wanafanya mazoezi Carrington wakati wachezaji wenzao wakiendelea na maandalizi ya msimu mpya huko Marekani.

Hadi sasa ni Marcus Rashford pekee kati ya wale waliotakiwa kuondoka ndio amepata timu akijiunga na Barcelona lakini wengine bado hakijaeleweka hadi sasa.

Man United inataka kuondoa baadhi ya wachezaji wake ili kupata fedha kwa ajili ya usajili mpya na pia hawapo katika mipango ya kocha.

Hata hivyo, Amorim amesisitiza kuwa bei lazima iwe sahihi kwa Mtendaji Mkuu, Omar Berrada na Mkurugenzi wa Michezo, Jason Wilcox la sivyo yupo tayari kuwarejesha kikosini.

"Tunawapa muda hawa wachezaji kufikiria na kuamua,” alisema Amorim.

"Kama tukifika hatua ya kuwa wanapaswa kujiunga na timu, watajiunga, kwa sababu bado ni wachezaji wetu. Najua kwa hakika Jason, Omar na klabu wana thamani waliyoiweka kwa wachezaji hawa. Ikiwa timu zinazowahitaji hazitafikia thamani hiyo, basi watabaki kuwa wachezaji wa Manchester United."

"Ninaelewa kwamba klabu nyingine zinangoja dakika za mwisho ili kuwasajili, lakini niseme tu zinaweza kupata mshangao. Niko tayari kuwapokea wachezaji tena kkosini. Ni kweli wanakutana na ushindani mkubwa wa namba hapa Man United, lakini ukiwa unataka kucheza Kombe la Dunia mwakani, unahitaji kupata mechi za kucheza kwa sabahu watakaporudi watapambana sana kuhakikisha wanacheza ili wasikose michuano hiyo."

Hadi sasa Man United imefanikisha usajili wa mastaa wawili kuboresha eneo lao la ushambuliaji ambao ni Matheus Cunha na Bryan Mbeumo.