Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim ana kazi ya kufanya Man United

AMORIM Pict

Muktasari:

  • Amorim anakiri kuwa Man United haiwezi kurudi kileleni kwa kutumia pesa nyingi kwenye usajili bali wanahitaji pia nguvu kutoka katika akademi zao hususani baada ya hali yao ya kiuchumi kuyumba.

MANCHESTER, ENGLAND: JUHUDI za Ruben Amorim kuifanya Manchester United icheze kwa mtindo wake zinaonekana kuwa na asilimia ndogo za kufanikiwa, kwani timu za akademi za mashetani wekundu hao  bado zinatumia mfumo wa kimbinu ambao hauendani na falsafa yake.

Amorim anakiri kuwa Man United haiwezi kurudi kileleni kwa kutumia pesa nyingi kwenye usajili bali wanahitaji pia nguvu kutoka katika akademi zao hususani baada ya hali yao ya kiuchumi kuyumba.

Kocha huyo wa Mashetani Wekundu yupo tayari kuendeleza utamaduni wa muda mrefu wa Old Trafford wa kutumia wachezaji vijana wa akademi  jambo ambalo aliwahi kufanya akiwa na Sporting Lisbon.

Hata hivyo, changamoto kubwa ni kwamba timu za vijana za United zinafundishwa kucheza mfumo wa 4-3-3 ambao Amorim hana imani nao kabisa.

Kocha huyo anakumbana na wakati mgumu zaidi kuwaingiza wachezaji chipukizi kwenye kikosi cha wakubwa kwa sababu wamelelewa kwenye mfumo tofauti wa kimbinu.

Wakuu wa akademi ya Man United wanasisitiza kuwa wanaendeleza wachezaji waliobora na wenye uwezo wa kuzoea aina yoyote ya mbinu, na Amorim tayari amewapa mechi za kwanza wachezaji chipukizi kama Harry Amass na Tyler Fredricson msimu huu.

Pia aliwajumuisha Dan Armer, Jaydan Kamason, Godwill Kukonki, Tyler Fletcher, Sekou Kone, Shea Lacey, Jack Moorhouse, na Jim Thwaites kwenye kikosi cha ziara yao ya maandalizi ya msimu waliyofanya Mashariki ya Mbali.

Hata hivyo, kuna pengo kati ya jinsi timu za vijana zinavyocheza na mfumo anaoutumia Amorim kwenye kikosi cha wakubwa.

Kocha huyo anaendelea kushikilia mfumo wake wa kutumia beki watatu na mabeki wa pembeni kushambulia kwa upana. Falsafa hiyo ndiyo iliyompatia mafanikio wakati akijijengea jina kama mmoja wa makocha bora barani Ulaya akiwa Braga na Sporting Lisbon.

Alikataa kabisa kubadilika licha ya kurithi kikosi cha Man United ambacho kinahangaika  kutekeleza mahitaji yake ya kiufundi tangu alipochukua usukani  Novemba mwaka jana.

Chanzo kimoja kilisema: “Amorim aliweka wazi alipokuwa akizungumza na Man United kuhusu ajira ya kuwa kocha wa timu hiyo, aliwaambia kwamba anahitaji uhuru wa kutumia mfumo aliotumia huko Ureno, lakini shida ni kwamba Sporting hata akademi yao awali inatumia mfumo wa 4-3-3, tofauti na Man United.”