Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim aambiwa hakuna kujitetea

AMORIM Pict

Muktasari:

  • Kocha huyo Mreno aliwasili Old Trafford, Novemba mwaka jana kuchukua mikoba ya Erik ten Hag, lakini alishindwa kutamba baada ya kikosi hicho kumaliza nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England na kuchapwa pia kwenye fainali ya Europa League.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim ameambiwa hakutakuwa na cha kujitetea tena msimu ujao kwa usajili utakaofanywa dirisha hilo na muda wa kuwa na timu pre-season.

Kocha huyo Mreno aliwasili Old Trafford, Novemba mwaka jana kuchukua mikoba ya Erik ten Hag, lakini alishindwa kutamba baada ya kikosi hicho kumaliza nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England na kuchapwa pia kwenye fainali ya Europa League.

Hiyo ina maana, hakutakuwa na michuano yoyote ya Ulaya huko Old Trafford msimu ujao, kitu ambacho Amorim alidai alipenda kitokee kwa sababu atakuwa na muda wa kukiandaa kikosi chake kwa michuano ya ndani kuliko kuwa na presha ya mechi za Ulaya.

Amorim alitua Man United na kutambulisha mfumo wa 3-4-3, ambao ulikuwa tatizo kwa sababu hakukuwa na idadi kubwa ya wachezaji wa kucheza staili hiyo.

Ashley Young sasa anasisitiza ni wakati wa kocha huyo kutuliza akili na kuweka mambo yake sawa ili kuthibitisha ni mtu sahihi katika kuifikisha mbele timu hiyo.

Staa huyo wa zamani wa Old Trafford alisema ishu ya kujitetea haitaeleweka tena kwa sasa kwa sababu atakuwa na muda wa kusajili na atakwenda kwenye pre-season kuandaa timu icheze kwa mtindo wake anaotaka, aliposema: "Nadhani Ruben Amorim ana staili yake, namna anavyofundisha, mbinu zake na anavyotaka timu iwe. Hakupaswa kuja kwa kipindi alichokuja, alipaswa kuja mwanzoni, si kama vile kuanza katikati kunakuwa na ugumu mkubwa.

"Nadhani alisema anahitaji kupewa muda, anahitaji madirisha mangapi ya usajili? Hatujui hilo. Lakini, anapaswa kuonyesha ubora wake muda mfupi tu msimu huu utakapoanza. Sidhani kama atahitaji kutoa visingizio tena. Afanye sasa kwa haraka, la itakuwa balaa kwake."

Shida inayomkabili Amorim hadi sasa ni kushindwa kupata wachezaji anaowataka kwa wakati. Ni Matheus Cunha pekee ndiye aliyesajiliwa hadi sasa kwenye dirisha hili akitokea Wolves, ambaye atakuja kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza. Dili la Bryan Mbeumo bado halijakamilika baada ya ofa zao mbili kukataliwa na Brentford. Man United inahitaji pia kipa na straika.

Mechi ya kwanza kwenye Ligi Kuu England itakabiliana na Arsenal, ambayo inafanya usajili wa kibabe, huku kipute hicho kitapigwa Agosti 17.