Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyesahaulika Man United afika fainali ya tatu

SANCHO Pict

Muktasari:

  • Aston Villa waliifunga Nottingham Forest kwa mabao 4-0 juzi baada ya kufanya 'comeback' kubwa katika nusu fainali, ikishuhudia nyota wake  John McGinn akifunga mawili huku Emi Buendia na Ollie Watkins wakikamilisha ushindi huo.

LONDON, ENGLAND: ASTON VILLA wamefuzu fainali ya kwanza ya mashindano ya klabu Ulaya baada ya miaka 44 huku kocha Unai Emery akitarajiwa kucheza fainali ya tano ya Europa League katika maisha yake ya ukocha.

Lakini, habari kubwa zaidi ni ya Jadon Sancho, nyota wa Manchester United ambaye sasa yupo njiani kucheza fainali ya tatu ya Ulaya mfululizo akiwa na klabu tofauti kila msimu. Mchezaji huyo anacheza kwa mkopo Villa.

Aston Villa waliifunga Nottingham Forest kwa mabao 4-0 juzi baada ya kufanya 'comeback' kubwa katika nusu fainali, ikishuhudia nyota wake  John McGinn akifunga mawili huku Emi Buendia na Ollie Watkins wakikamilisha ushindi huo.

SANCH 01

Sancho mwenye umri wa miaka 26, ambaye yupo Aston Villa kwa mkopo kutoka Manchester United anaweza kuingia majira ya kiangazi bila klabu rasmi licha ya mafanikio hayo. Mkataba wake Villa utaisha Juni 30 na bado hajui mustakabali wake. Hata hivyo, ana nafasi ya kushinda taji la Ulaya kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kushinda Conference League akiwa Chelsea msimu uliopita chini ya kocha Enzo Maresca.

SANCH 02

Kabla ya hapo aliifikisha Borussia Dortmund fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya miezi michache tu baada ya kuondoka Manchester United kwa mkopo Januari 2024. Sancho alianza fainali dhidi ya Real Madrid iliyopigwa dimba la Wembley na kucheza dakika 87 licha ya Dortmund kupoteza 2-0. Mafanikio hayo yanaweza kumsaidia kupata timu mpya majira yajayo ya kiangazi.