Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Alexander Isak aachwa safari ya Singapore

ISAAK Pict

Muktasari:

  • Fowadi huyo wa Sweden mwenye umri wa miaka 25, alikuwa akihusishwa na uhamisho wa pesa nyingi kwenda Liverpool kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.

NEWCASTLE, ENGLAND: STRAIKA, Alexander Isak amepigwa chini kwenye kikosi cha Newcastle United kilichosafiri kwenda Singapore kwenye ziara yao ya mechi za pre-season.

Fowadi huyo wa Sweden mwenye umri wa miaka 25, alikuwa akihusishwa na uhamisho wa pesa nyingi kwenda Liverpool kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Staa huyo alifanya mazoezi na wenzake kwenye kambi ya pre-season huko Austria mapema mwezi huu, lakini alirudishwa nyumbani na kocha Eddie Howe baada ya ishu hiyo ya kuwindwa na Liverpool na kosha huyo alisema angekuwamo kwenye ziada ya huko Asia.

Lakini, Liverpool iliamua kwenda kumnasa straika Hugo Ekitike kwa Pauni 79 milioni na kuachana na Isak, baada ya kujibiwa na Newcastle kwamba hauzwi.

Jambo la kutakiwa na Liverpool linadaiwa kumvuruga Isak kiasi cha kuharibu mazungumzo yao ya kuhusu mkataba mpya huko St James' Park.

Newcastle imedai kwamba Isak atakosa ziara hiyo ya huko Asia kutokana na kuwa majeruhi. Mkataba wa sasa wa mkali huyo umebakiza miaka mitatu.

Analipwa mshahara wa Pauni 130,000 kwa wiki, lakini kinachoelezwa ni kwamba kwa sasa anataka alipwe Pauni 300,000 kwa wiki.

Newcastle itakipiga na Arsenal huko Singapore, Jumapili. Kikosi hicho cha Newcastle kisha kitasafiri kwenda Korea Kusini, ambako kitacheza mechi dhidi ya K-League XI na Tottenham. Mechi yao ya nyumbani kwenye kujipima nguvu itakuwa dhidi ya Espanyol, itakayopigwa St James' Park, Agosti 8.


MAVITU YA ISAK HUKO EPL 2024-25

-Amecheza: Mechi 34

-Ametengeneza: Nafasi 42

-Amepiga: Pasi 658

-Amefunga: Mabao 23

-Ametoa: Asisti 6

-Amelenga golini: Mashuti 46