Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ajax yaendelea kusuasua, Benfica ikipata ishindi wa kwanza UEFA

AJAX PICT

Muktasari:

  • Klabu hiyo ya Uholanzi imekuwa katika hali mbaya barani Ulaya, ikiwa ni kipigo chao cha tano mfululizo katika mashindano ya msimu huu, baada ya kupoteza mechi tatu mfululizo pia kwenye Europa League msimu uliopita.

AMSTERDAM, UHOLANZI: MATESO ya Ajax katika Ligi ya Mabingwa Ulaya yameendelea baada ya kuchapwa na Benfica, timu nyingine iliyokuwa ikipambana, na kuiacha Ajax mkiani mwa msimamo wa kundi.

Klabu hiyo ya Uholanzi imekuwa katika hali mbaya barani Ulaya, ikiwa ni kipigo chao cha tano mfululizo katika mashindano ya msimu huu, baada ya kupoteza mechi tatu mfululizo pia kwenye Europa League msimu uliopita.

Benfica, iliyokuwa imepoteza mechi sita mfululizo, hatimaye usiku wa Novemba 25, 2025 imepata ushindi wa kwanza katika Ligi ya Mabingwa chini ya kocha José Mourinho.

Klabu hiyo ya Ureno ilifungua ukurasa wa mabao katika dakika ya sita kupitia shuti kali kutoka kwa Samuel Dahl.

Ajax iliyokuwa nyumbani pale Johan Cruijff ArenA, ilipata nafasi kadhaa za kusawazisha, lakini kipa Anatoliy Trubin aliokoa mashambulizi ya Davy Klaassen na Rayane Bounida.

Oscar Gloukh pia alikaribia kufunga kwa shuti kali, lakini Trubin alizuia mpira huo kwenye mwamba wake wa karibu huku Ajax ikiendelea kusaka bao la kusawazisha.

Hata hivyo, Benfica ilifunga bao la pili katika dakika za nyongeza na kufanikisha ushindi huo muhimu, kupitia mkwaju mkali wa Leandro Barreiro aliyeingia kwenye boksi na kumalizia kwa ustadi.

Wakati Benfica ikifufua matumaini ya kufuzu hatua ya mtoano ambapo baada ya kukusanya pointi za kwanza, Ajax sasa iko katika hatari kubwa ya kuaga mashindano hayo mapema ikiwa haijapata pointi hata moja huku ikifunga bao moja pekee katika mechi tano ilizocheza.

AJ 01

GALATASARAY YADUWAZWA KWAO
Pale Rams Park jijini Istanbul nchini Uturuki, Galatasaray ikiwa nyumbani iliduwazwa na Union Saint-Gilloise katika mechi nyingine ya mapema UEFA iliyochezwa Novemba 25, 2025.

Promise David aliifungia Union Saint-Gilloise bao pekee katika ushindi huo na kuvunja rekodi yao ya kupoteza mechi tatu mfululizo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mshambuliaji huyo wa Canada, alifunga katika dakika ya 57 akimalizia pasi ya kurudi ya Adem Zorgane, moja kati ya nafasi chache zilizotengenezwa na timu zote mbili kwenye mechi hiyo iliofanyika Uturuki.

Katika kipindi cha kwanza, timu zote zilikaribia kufunga baada ya kugonga mwamba, kiungo wa Galatasaray, Gabriel Sara alipiga shuti kali la yadi 25 lililogonga mlingoti, kabla ya nahodha wa Union, Christian Burgess, kuona mpira wake wa kichwa ukigonga mtambaa wa panya.

Galatasaray ilionekana kukosa makali hasa kutokana na kukosekana kwa mshambuliaji nyota Victor Osimhen, ambaye mpaka sasa ndiye kinara wa mabao kwenye mashindano haya akiwa nayo sita.

Wachezaji wa zamani wa Manchester City, Ilkay Gundogan na Leroy Sane, walikuwa kimya kwa sehemu kubwa ya mechi hiyo, sambamba na Mauro Icardi, mshambuliaji wa zamani wa Inter Milan na Paris Saint-Germain.

Kufuatia kipigo hicho kwa Galatasaray, timu hiyo imesalia na pointi tisa hiku Union ikiwa nazo sita, zote zikishuka dimbani mara tano.