Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kigari cha Neymar ‘chazua gumzo’ Marekani

KIGARI Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo wa zamani wa Barcelona alionekana katika hifadhi hiyo Alhamisi, kufuatia kipigo cha mabao 2-1 ambacho Brazil ilipata dhidi ya Norway.

NEW YORK, MAREKANI: NYOTA wa Brazil, Neymar ameonekana akitumia kigari 'skuta ya umeme' katika Hifadhi ya Burudani ya Universal Orlando Resort nchini Marekani, siku chache tu baada ya Brazil kuondolewa kwenye Kombe la Dunia.

Nyota huyo wa zamani wa Barcelona alionekana katika hifadhi hiyo Alhamisi, kufuatia kipigo cha mabao 2-1 ambacho Brazil ilipata dhidi ya Norway.

Neymar, ambaye ndiye kinara wa mabao wa muda wote wa Brazil akiwa na mabao 80, katika video iliyosambaa mitandaoni, Neymar anaonekana akiwa amevalia kaptura ya kijivu, fulana yenye rangi nyeusi na nyeupe, pamoja na kofia na miwani ya jua, huku akiendesha skuta hiyo ya umeme kuzunguka ndani ya hifadhi.

Wakati akipita akiwa amezingirwa na walinzi wake, nyota huyo aliwasalimia mashabiki kwa kuonyesha alama ya dole gumba juu.

Shuhuda mmoja aliyezungumza amesemamwanzoni watu wengi hawakugundua kuwa aliyekuwa kwenye skuta alikuwa Neymar, lakini muda mfupi baadaye alitambuliwa na mashabiki wakaanza kumzunguka.

"Mwanzoni hakuna aliyegundua ni yeye. Baadaye ndipo watu walipoanza kumzingira," alisema.

Aliongeza: "Sijui kwa nini alikuwa anatumia skuta, lakini hali ya hewa ilikuwa ya joto kali sana. Tulikuwa kwenye mgahawa sehemu nyingine ya hifadhi, kisha tukawasikia walinzi wakimtaja Neymar, ndipo tukamfuata. Tulipofika walidhani sisi ni sehemu ya ulinzi, hivyo tukabaki karibu naye."

Muonekano huo wa Neymar unakuja siku chache baada ya kutangaza rasmi kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya Brazil kufuatia kuondolewa kwa Selecao kwenye Kombe la Dunia.

Baada ya kipenga cha mwisho katika mchezo dhidi ya Norway, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34 alionekana akitokwa na machozi uwanjani kabla ya kufarijiwa na wenzake, akihitimisha safari yake ya kimataifa kwa huzuni.