Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Geita yamtaka winga Yanga

Muktasari:

  • Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa timu hiyo, umeliambia Mwanaspoti Edmund ni miongoni mwa wachezaji wanaopigiwa hesabu za kujiunga na kikosi hicho, ingawa makubaliano yaliyopo na Yanga ni kumpata mchezaji huyo kwa mkopo na sio kumnunua.

MABOSI wa Geita Gold wamefungua mazungumzo na mabingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2025-2026, Klabu ya Yanga kwa lengo la kumrejesha aliyekuwa winga nyota wa kikosi hicho, Edmund John kutokana na kutopata nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa timu hiyo, umeliambia Mwanaspoti Edmund ni miongoni mwa wachezaji wanaopigiwa hesabu za kujiunga na kikosi hicho, ingawa makubaliano yaliyopo na Yanga ni kumpata mchezaji huyo kwa mkopo na sio kumnunua.

"Edmund ni miongoni mwa wachezaji tunaoamini wanaweza kutusaidia kwa msimu ujao kutokana na uzoefu wake na isitoshe pia Geita ni nyumbani, makubaliano yaliyopo ni ya mkopo kwa sababu hatutaweza kuvunja mkataba wake," kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kilisema uzoefu wa mchezaji huyo ni chachu ya kuongeza ushindani msimu ujao, ambapo kwa sasa mabosi wa timu hiyo wamejipanga kuongeza wachezaji wengi watakaoleta morali ya kukipambania kikosi hicho katika mashindano mbalimbali.

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Geita Gold, Zubery Katwila aliyeipandisha timu hiyo daraja kutoka Championship hadi Ligi Kuu Bara, alisema baada ya msimu wa 2025-2026, kumalizika alitoa mapendekezo yake yote kwa ajili ya kufanyiwa kazi haraka.

Edmund aliwahi kuitumikia Geita Gold msimu wa 2023-2024, huku akikumbukwa zaidi baada ya kuifungia timu hiyo bao moja la Ligi Kuu, katika ushindi wa kikosi hicho wa 1-0, dhidi ya maafande wa JKT Tanzania, mechi iliyopigwa, Novemba 22, 2023.

Kiwango bora alichokionyesha nyota huyo, kikawavutia mabosi wa Singida Black Stars iliyomsajili kwa msimu wa 2024-2025 na Agosti 14, 2025, alijiunga rasmi na Yanga, ingawa amekosa nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza kutokana na ushindani. 

Geita iliyoshuka daraja msimu wa 2023-2024, imerejea Ligi Kuu baada ya kutwaa taji la Championship msimu wa 2025-2026 na pointi 77, nyuma ya Kagera Sugar iliyomaliza nafasi ya pili na pointi 72, ikirejea kufuatia kushuka msimu wa 2024-2025.