Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

AFCON 2025 beki chagua bega Diallo au Zaha   

Muktasari:

  • La, mashabiki watavutiwa na vita gani kwenye Kundi F? Au ile ya Bryan Mbeumo wa Cameroon na Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon? Ni kivumbi na jasho kwenye mchakamchaka huo wa AFCON.

CASABLANCA, MOROCCO: CHAGUA mwenyewe bega, unataka kumkabili Amad Diallo au Wilfried Zaha. Hilo swali linawahusu mabeki wa Msumbiji, Jumatano ya leo huko Morocco kwenye mikikimikiki ya AFCON 2025.

La, mashabiki watavutiwa na vita gani kwenye Kundi F? Au ile ya Bryan Mbeumo wa Cameroon na Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon? Ni kivumbi na jasho kwenye mchakamchaka huo wa AFCON.

Huko Stade de Marrakech, Ivory Coast ya wakali matata kama Amad na Zaha watakuwa bize kuwauliza maswali magumu mabeki wa Msumbiji katika mechi yao ya kwanza ya hatua ya makundi ya Afcon 2025 kwenye Kundi F, ambalo pia litashuhudia mchezo mwingine baina ya Cameroon na Gabon. Mambo ni moto.

Simba Wasioshindika yenye kikosi kilichojaa mastaa kibao, inaamini itakuwa kwenye mikono salama ikiongozwa na mkali Mbeumo, lakini hiyo ya Stade Adrar haitakuwa nyepesi kwao kwa sababu watakabiliana na Gabon yenye mastaa wa maana, akiwamo straika Aubameyang.

Mechi hizo mbili zinazotabiriwa kuwa na upinzani mkali uwanjani zote zitafanyika usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Lakini, mapema kabisa, kutakuwa na kasheshe jingine na staa aliyejizolea umaarufu mkubwa kwenye soka la Tanzania, Stephane Aziz Ki atashuka uwanjani Stade Mohamed V na kikosi chake cha Burkina Faso kukabiliana na Equatorial Guinea katika mchezo wa Kundi E wa mikikikimikiki hiyo ya Afcon 2025 inayozidi kupamba moto huko Morocco.

Mechi nyingine ya kundi hilo itakuwa huko uwanjani Moulay Hassan, wakati Riyad Mahrez atakapowaongoza mabingwa wa zamani wa Afcon kuonyeshana ubabe na Sudan katika kusaka pointi za kwanza katika harakati zao za kunyakua taji hilo la ubingwa wa Afrika wakati wa mashindano hayo yakifanyika kwa mara ya 35.

Mashindano ya Afcon 2025 yamezidi kunoga huko Morocco na Taifa Stars ilirusha kete yake ya kwanza usiku wa jana Jumanne katika kipute kilichofanyika uwanjani Fez dhidi ya Nigeria. Kilichotokea kimetokea katika mechi hiyo ya Kundi C, lililoshuhudia pia mechi nyingine na Uganda ilikipiga na Tunisia.