Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Adingra asononeka kukosa Afcon 2025

ADINGRA Pict

Muktasari:

  • Winga huyo wa Sunderland alifunguka pia kuhusu ushauri aliopewa na mchezaji mwenzake wa Ivory Coast, Amad Diallo.

CASABLANCA, MOROCCO: STAA wa Ivory Coast, Simon Adingra amefunguka juu ya huzuni yake ya kuwekwa kando katika kikosi cha Tembo kinachoshiriki mashindano ya Afcon 2025 huko Morocco.

Winga huyo wa Sunderland alifunguka pia kuhusu ushauri aliopewa na mchezaji mwenzake wa Ivory Coast, Amad Diallo.

Adingra alikiri kufunga bao lake la kwanza mbele ya mashabiki wa Sunderland uwanjani Stadium of Light kulimsaidia kumwondoa kwenye kipindi kigumu kilichokuwa kinamkabili baada ya kutoswa na Ivory Coast kwenye kikosi cha Afcon 2025.

Winga huyo alifunga bao hilo dhidi ya Leeds United na kusema: “Kilikuwa kitu kizuri kufunga mbele ya mashabiki wetu, kwanza bao langu la kwanza Sunderland, najisikia vizuri. Nilikuwa na kipindi kigumu mwanzoni mwa msimu. Ilikuwa changamoto kubwa kwangu leo, lakini hapa nimetumia nafasi yangu. Natumai nitaendelea kufanya hivyo.”

Adingra alifunguka kuhusu huzuni ya kuwekwa kando katika kikosi cha Ivory Coast kilichopo kwenye mashindano ya Afcon 2025, akisema: “Ndiyo, kilikuwa kipindi cha huzuni sana kwa kutokuwapo kwenye timu yangu ya taifa. Kilikuwa kipindi kigumu sana. Lakini, ipo wazi, usipocheza kwenye klabu yako huwezi kuitwa kwenye timu ya taifa. Afcon iliyopita, nilikuwapo na kushinda ubingwa na timu yangu ya taifa, nilitarajia kuwapo na hii, lakini imekuwa tofauti.”

Adingra amesema mchezaji wa zamani wa Sunderland, aliyewahi kucheza hapo kwa mkopo Amad Diallo amekuwa akimshauri mambo mengi ikiwamo kuzoea mazingira ya huko Wearside.