Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Acheni tu waje...

LONDON, ENGLAND. TUNAENDELEA tulipoishia. Chama lako lilikuwa namba ngapi vile?  Wikiendi hii miamba ya soka England inaingia uwanjani  baada ya mapumziko ya wiki mbili kupiusha ratiba ya Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) kwa mechi za kimataifa kupigwa na nchi mbalimbali zilikuwa bize na timu zao za taifa.

Huku mechi kubwa ya wikiendi ikisubiriwa leo kati ya Manchester City na Liverpool, presha kubwa iko kwa Pep Guardiola na kikosi chake kwani ina mtihani wa kushinda mchezo huo ili kuendelea kusalia nafasi ya kwanza na ikipoteza tu, inaweza ikajikuta nafasi ya nne au tano.

Mabingwa hao watetezi watakuwa dimbani Etihad kuikaribisha Majogoo wa Liverpool na kwenye msimamo wa ligi zinatofautiana pointi moja tu City akiongoza na 28 na Liverpool 27.

Hii ina maana Liverpool yenye pointi sawa na Arsenal (27), ikishinda mchezo huo itaishusha City na kupanda kileleni, huku michezo mingine inayozihusu timu nne za juu (top four) ikiamua hatma ya City kileleni.

City ilitoka sare ya mabao 4-4 na Chelsea mchezo wa mwisho kabla ya kwenda mapumziko na ingeshinda ingejiwekea mazingira mazuri kileleni, huku Liverpool ambao walionekana kuanza kwa kusuasua wamerudisha upinzani kwenye vita ya ubingwa na mchezo wa mwisho ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Brentford.

Arsenal itakuwa ugenini kwa  Brentford leo na ushindi utazidi kuipaisha kwenye msimamo na endapo City na Liverpool zitatoka sare inaweza ikapanda na kuondoza msimamo.

Arsenal licha ya kukabiliwa na wachezaji majeruhi kama Gabriel Jesus, Martin Odegaard, Ben White, Jorginho na Thomas Partey imeendelea kuwa imara zaidi na Kocha Mikel Arteta amepania kuendeleza ushindi mfululizo licha ya kuwa na wachezaji majeruhi wengi kwenye kikosi chake.

Baada ya kufungwa mechi mbili mfululizo Tottenham Hotspurs inarejea ikiwa na matumaini ya kupata ushindi na itacheza dhidi ya Aston Villa.

Ukingalia kwenye msimamo wa ligi timu hizo zimepishana kwa pointi moja tu, Spurs ina pointi 26 ikiwa nafasi ya nne huku Aston Villa ikiwa na pointi 25 nafasi ya tano. Ni wazi mechi hiyo itakuwa na ushindani mkubwa.

Aston Villa imekuwa imara msimu huu, katika michezo mitatu ya mwisho iliyocheza haijapoteza mechi hivyo, huku Spurs ikichezea vichapo mfululizo.

Chelsea iliwatibulia Spurs na kuibamiza mabao 4-1 kabla ya kufungwa na Wolves mabao 2-1.

Kocha wa Ange Postecoglou anakabiliwa na majeruhi wengi kwenye kikosi chake na ataendelea kuwakosa Ivan Perisic, Destiny Udogie, James Maddidon, Micky van de Ven, Ryan Sessegnon, Richarlison na Manor Solomon.

Pia baadhi ya nyota wake wanatumikia adhabu za kadi kama Sergio Romero na Yves Bissouma.

Manchester United inazidi kujitafuta baada ya kusuasua na ilipanda hadi nafasi ya sita ikiwa na pointi 21, na itashuka uwanja wa Goodison Park kuikabili Everton.

Kocha Erik ten Hag anakabiliana na timu ambayo hivi karibuni ilipokwa pointi 10 na Chama cha soka England (FA) kutokana na kukiuka sheria za matumizi ya pesa michezoni.

Pia ana majeruhi wengi, lakini taarifa njema ni kurejea kwa Luke Shaw baada ya kukaa nje ya dimba kwa muda mrefu. Man United itawakosa Lisandro Martinez, Casemiro, Tyrell Malacia, Jonny Evans, huku Andre Onana akiwa hatihati kwani alipata majeraha akiwa katika majukumu ya kimataifa.

Kwa sasa Everton ipo nafasi ya 19 ikiwa na pointi nne inajivunia kuwa nyumbani na itajaribu kusaka pointi tatu muhimu ili kuchomoka nafasi iliyopo.

Everton katika mechi tatu za mwisho ilishinda mara mbili na kutoka sare moja, hivyo inawapa kazi nyingne ya kuhakikisha inachomoka chini ili kuekupa kushuka daraja msimu ujao.

Wakati huo huo, Newcastle yenye pointi 20 inainyemela Man United nafasi ya sita ambayo ina pointi 21, kwa tofauti ya pointi moja kwenye msimamo na matokeo ya mechi ya zao leo itabadili kila kitu, itakuwa uwanjani leo dhidi ya Chelsea iliyokuwa nafasi ya 10 kwa pointi 16. Vile vile bila kuisahau Brighton yenye ppointi 19 nafasi ya nane itakuwa dimbani ikicheza dhidi ya Nottingham Forest imepisha na Newcastle na Man United kwa pointi chache.

Kikosi cha Mauricio Pochettino licha ya kusuasua lakini ilizinduka na kuzishangaza Arsenal na Man City kwani iliwazamisha sare kila mmoja. Endapo itapata ushindi dhidi ya Newcastle inaweza kupanda nafasi ya tisa lakini lazima iwaombee njaa West Ham ambayo itamenyana na Burnley.