Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

 The King is back!

Muktasari:

  • Lakini, unajua kwanini jamaa alicheka? Sikia, bado hajavunja rekodi yoyote ya maana hadi sasa katika umri alionao wa miaka 27 ikilinganishwa na LeBron mwenye miaka 40 ambaye tayari keshavunja karibu rekodi 50 zilizowahi kufanywa na wakongwe waliostaafu kitambo.

LOS ANGELES, MAREKANI: AUSTIN Reaves amecheeekaaa kuhusu LeBron James kuvunja rekodi kibao za Ligi ya Kikapu Marekani (NBA), na hasa baada ya hivi karibuni kupatwa na majeraha. Na kilichonfanya acheke ni kuambiwa hata yeye atazifikia na kuzivuka rekodi hizo za mchezaji mwenzake katika taaluma yao kikapu.

Lakini, unajua kwanini jamaa alicheka? Sikia, bado hajavunja rekodi yoyote ya maana hadi sasa katika umri alionao wa miaka 27 ikilinganishwa na LeBron mwenye miaka 40 ambaye tayari keshavunja karibu rekodi 50 zilizowahi kufanywa na wakongwe waliostaafu kitambo.

LeBron karejea uwanjani baada ya kuwa nje akijiuguza kutokana na majeraha na wiki hii alikuwa uwanjani kukipiga dhidi ya Utah Jazz nyumbani katika mchezo ambao mashabiki walipania kuiangalia safu ya ushambuliaji ilivyokuwa bize uwanjani chini ya uongozi wake ikiwachapa wapinzani wao kwa pointi 140 -126.

Lakini, kinachoelezwa ni kwamba licha ya kutoonyesha maajabu makubwa katika mchezo huo, LeBron aliibua shangwe kubwa kwa mashabiki wa mchezo huo ikizingatiwa kwamba ndiye staa mkubwa kuliko wote wa kikapu Marekani kwa sasa.

KIJEMBE CHA REAVES

Wakati Lakers ikijiandaa kwa mchezo mwingine wa pili ugenini dhidi ya Utah Jazz utakaopigwa leo usiku kuamkia kesho staa anayechupukia wa timu hiyo haishiwi vituko kwani kikosini wachezaji wanamchukulia kwamba ndiye anayewapa burudani ya vichekesho wanapoboreka.

Katika mazoezi Reaves alipoulizwa na waandishi wa habari juu ya LeBron, alitupa kijembe kuwa "mwenye nyumba amerudi", na sasa waliokuwa wakijiona wafalme wanyamaze.

Lakini, alikuwa ni Luka Doncic aliyeishia kushangilia zaidi kwani tangu alipoumia LeBron na kuwa nje kwa miezi miwili na ushei, Lakers ilimtegemea yeye kuichezesha timu uwanjani na hivyo kurudi kwa mwamba ni ishara kwamba mzigo kwake utapungua.


AANZA KUFANYA MAMBO

LeBron alicheza mchezo dhidi ya Utah Jazz akitoka kukosa mechi mechi 14 za mwanzo wa msimu kutokana na maumivu ya sciatica (maumivu yanayotoka sehemu ya chini ya mgongo na kusafiri kupitia nyonga, makalio hadi mguuni kupitia mshipa unaoitwa sciatic nerve).

Katika mchezo huo alitupia pointi 11, asisti 12 na kuzuia mitupo ya wazi mitatu ndani ya dakika 30 pekee alizocheza kwenye mechi iliyokuwa na msisimko mkubwa katika misimu 23 mfululizo ya NBA akivunja rekodi ya Vince Carter ya misimu 22.

Mitupo yake miwili ya mafanikio ya mbali (three-pointers), pia imemuweka juu ya Reggie Miller akichukua nafasi ya sita kwenye orodha ya muda wote ya NBA ya wachezaji waliofunga three-pointers nyingi zaidi.

Bila shaka morali iko juu kwa Lakers wenye rekodi ya 11–4, ambao kwa sasa wana rekodi ya tatu bora katika NBA msimu huu. Lebron na Reaves wamekuwa na muunganiko mzuri  uwanjani msimu huu, lakini inaonekana Reaves ana kazi ya ziada kama anataka urafiki huo uhamie nje ya uwanja, kwani Doncic ni mtu anayependa mambo ya kivyakevyake asiyependa kujichanganya kilabu nyakati za usiku, tabia aliyonayo Reaves.