Super League yapandisha thamani hisa za Juventus, Man United

Monday April 19 2021
hisa pc

ROMA, ITALIA.

Thamani ya hisa za Juventus na Manchester United zimepanda leo baada ya klabu hizo kutangaza kushiriki michuano mipya ya Super League ya Ulaya pamoja na klabu nyingine kumi vigogo.

Hisa za klabu hiyo ya Italia zilipanda kwa asilimia saba hadi kufikia Euro 0.827 (sawa na Sh2,308 za Kitanzania) baada ya kufunguliwa katika soko la hisa la Milan.

Hiyo ni baada ya wiki kadhaa za bei ya hisa za Juventus kuporomoka tangu ilipoondolewa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya mwezi Machi.

Hisa za Manchester United, ambayo imeandikishwa katika soko la hisa la New York, zilipanda kwa asilimia tano kabla ya kuanza kuuza.
Klabu hizo mbili zilitangaza kutihibitisha kushiriki michuano hiyo mipya pamoja na klabu nyingine kutoka Italia, Hispania na England.

Inter Milan, AC Milan, Liverpool, Arsenal, Chelsea, Manchester City, Tottenham, Barcelona, Real Madrid na Atletico Madrid pia zimetia saini mpango huo, ambao umeibua ukosoaji mkubwa kutoka mamlaka za soka, mashabiki na wachambuzi.

Advertisement
Advertisement