Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simeoni: Namchagua Messi sio Ronaldo

Muktasari:

Kocha Simeone aliyeipa Atletico Madrid mafanikio makubwa asema kuwa Messi ni mchezaji mwenye kila kitu.

Madrid, Hispania. Kocha wa timu ya Atletico Madrid, Diego Simeone, amesema kuwa ataendelea kuamini kuwa kwake mchezaji bora wa sasa duniani ni Lionel Messi na sio Cristiano Ronaldo.
Simeone Kocha aliyeipa Atletico Madrid mafanikio makubwa alisema kuwa Messi ni mchezaji mwenye kila kitu na shabiki wa kweli wa soka anatamani kumuona mchezaji huyo kila mara akiwa na mpira.
Alisema tofauti na Ronaldo nahodha huyo wa Argentina anajua kuuchezea mpira na kuufanya anavyotaka kiasi kwamba ni burudani kumtizama.
Alisema utashi na mtazamo wake haupo kwa sababu Messi ni Muargentina mwenzake bali kutokana na kile anachokifanya uwanjani.
Alisema ingawa Argentina, iliishia robo fainali ya Kombe la Dunia 2018 kwa kufungwa na Croatia lakini mchango na juhudi binafsi wa Messi ndio ziliifikisha timu hatua hiyo.
Simeone aliyasema hayo katika kumjibu msaidizi wake katika klabu ya Atletico, German Burgos, ambaye alimponda Messi kutokana na Argentina kutolewa na Croatia katika fainali za Kombe la Dunia.