Rio amshika sikio Haaland

Friday November 26 2021
Halaand PIC

LONDON, ENGLAND. RIO Ferdinand anaamini nyota wa Borussia Dortmund, Erling Haaland atakuwa moto wa kuotea mbali endapo kama atajiunga na Liverpool badala ya Manchester City.

Beki huyo wa zamani wa Manchester United, amemtazama Haaland na timu atakayofiti kucheza siku za usoni, akiondoka Dortmund na kutua Ligi Kuu England.

“Kama ningekuwa Liverpool, ningemchukua mara moja Haaland, akicheza hapa sehemu ya ushambuliaji ya Liverpool itakuwa hatari sana, sidhani kama atashindwa kufiti kwa haraka, kucheza Liverpool mfumo wake sio mgumu, nadhani Haaland ataweza,” alisema Rio.

Haaland aliukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, kutokana na majeraha wakati Dortmund ilipocheza dhidi ya Sporting Lisbon na kupokea kichapo cha mabao 3-1, kilichowang’oa kwenye michuano hiyo.

Haaland anawindwa na timu vigogo Ulaya kama Real Marid, Manchester United, Chelsea, Barcelona na Manchester City.

Advertisement