Man City bado ipo ipo sana kuisaka saini ya Kane

Friday December 31 2021
Kane PIC

MABOSI wa Manchester City wamepanga kuwasiliana tena na Tottenham katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ili kuipata huduma ya straika wa timu hiyo na England, Harry Kane.

Man City ilihitaji sana kumsajili staa huyo katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi lakini Spurs iligoma kabisa kumuuza licha ya kiasi kikubwa cha pesa kilichowekwa mezani.

Man City kwa sasa inaonekana kuwa na ulazima wa kupata straika kwa sababu mastraika waliokuwepo wamekuwa wakisumbuliwa sana na majeraha ya mara kwa mara.

Hata hivyo hawana presha kubwa kwenye kufanikisha mchakato huo kwa sababu timu yao imekuwa ikifunga mabao ya kutosha licha ya kukosekana kwa straika asilia. kataba wa sasa wa fundi huyo unatarajiwa kumalizika mwaka 2024.

Advertisement