Griezmann awekewa mchongo Man United

Griezmann awekewa mchongo Man United

MANCHESTER ENGLAND. HABARI ndo hiyo. Manchester United imeripotiwa kufanya jaribio la kunasa saini ya Antoine Griezmann kwenye dirisha lililopita na huenda wakarudi tena Januari kukamilisha mpango wa kumsajili Mfaransa huyo.

Griezmann kwa sasa anakipiga Atletico Madrid kwa mkopo akitokea Barcelona na Man United ilitaka saini yake kwenye dirisha lililopita walipokuwa wakisaka huduma ya mshambuliaji wa kati baada ya Cristiano Ronaldo kuwatishia kuondoka.

Griezmann alikuwa mchezaji wa Barca tangu 2019 aliponaswa kutoka Atletico kwa ada ya Euro 120 milioni. Hata hivyo, baada ya miaka miwili ya panda shuka huko Nou Camp, amerudi zake Wanda Metropolitano kwa mkopo.

Griezmann anaweza kunaswa jumla na Atletico kwa ada ya Euro 40 milioni na kuna makubaliano, ambayo yanawafanya Atletico kumtumia mchezaji huyo kwa dakika chache uwanjani. Kuna timu nyingine za England zinamtaka pia Griezmann.

Atletico inamtumia Griezmann kwa dakika zisizozidi 30 kwenye kila mechi ili kukwepa ishu ya kuwalipa Euro 40 milioni Barca.

Staa huyo anaripotiwa kuchoka jambo hilo na huenda akafikiria kuachana na Atletico kwenye dirisha la Januari. Na hilo ndilo linalofichua kwamba Man United wanaweza kurudi vitani Januari kwenda kunasa saini yake.