Arteta awaka kadi ya Pepe

Arteta awaka kadi ya Pepe

London, England. Mikel Arteta ameponda kadi nyekundu aliyoonyeshwa winga wake, Pepe, akidai kuwa hakukuwa na mgusano wowote aliposhutumiwa kumpiga kichwa Ezgjan Alioski wa Leeds.

Kocha huyo wa Arsenal alifanikiwa kucheza pungufu na kulazimisha sare ugenini dhidi ya kikosi cha kocha Marcelo Bielsa, licha ya kucheza hivyo kwa dakika 40.

Tukio hilo la kadi nyekundu lilitokea mapema kipindi cha pili, na baada ya VAR kuangalia, winga huyo Pepe alionyeshwa kadi ya moja kwa moja iliyomtoa njje kwenye Uwanja wa Elland Road.

Baada ya mchezo huo kumalizika, Arteta hakusita kuonyesha hasira yake juu ya kadi hiyo na kumlaumu mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Alioski kwa kukuza tukio hilo.

Arteta aliiambia BBC: “Tukio kama hili halikubaliki. Ni kweli halikubaliki.

Katika kiwango kama hiki cha Ligi Kuu, hutakiwi kufanya hivi.”

Kuhusu matokeo ya mchezo huo, Arteta aliongeza: “Kutokana na kumpoteza Pepe mapema katika mchezo ule, tuliamua kukubaliana na hali.

“Huwa sipendi kupata sare, lakini likishatokea hakuna namna, tumepata pointi moja. Haikubaliki.

“Kipindi cha kwanza tulicheza katika vipindi viwili. Mchezo kama kuna wakati ulivunjika, tulianza kupoteza mipira kirahisi na kuwapa nafasi fulani ya kutushambulia.

“Kipindi cha pili kilikuwa na kila mbinu ya kujilinda vizuri na kuwa watulivu kwa kutumia mianya michache ambayo ilikuwa ikiachwa kwa ajili ya kushambulia.”

Beki mkongwe wa Manchester United, Patrice Evra alikuwa mchambuzi katika mchezo huo kwenye kituo cha Sky na kusema kuwa Pepe alitakiwa kukiomba radhi kikosi cha Arsenal.

Licha ya kumtaka nyota huyo kuwaomba radhi wenzake, pia beki huyo wa zamani wa kushoto anadhani kuwa Alioski alilikuza mno suala la kupigwa kichwa na kumsababishia mwenzake kadi.

Evra alisema: “Pepe anatakiwa kusema samahani kwa wenzake.”