Allison: Kombe la FA ni mipango yetu

Friday May 13 2022
FA PIC

LIVERPOOL, ENGLAND. KIPA wa Liverpool, Allison Becker amesisitiza wamepania kubeba ndoo ya FA kesho kwenye mechi ya fainali hiyo dhidi ya Chelsea itakayochezwa uwanja wa Wembley.

Liverpool tayar imeshaweka kabayi mataji megine kama Ligi Kuu England, Carabao, Super Cup na Kombe la dunia kwa ngazi ya klabu tangu Jurgen Klopp alipoteuliwa kuwa kocha mwaka 2015.

Lakini kipa huyo anaamini bado wana deni kwa kocha wao na wana shauku kubwa ya kumfunga Chelsea kwenye fainali hiyo hiyv hautakuwa mchezo rahisi kwa upande wa The Blues.

Mbali na fainali hiyo ya FA vijana wa Klopp wametinga fainali ya Ligi Mabingwa Ulaya na itachuana vikali na Real Madrid kwenye mechi hiyo itakayopigwa Mei 28 jijini Paris, Ufaransa.

Akizungumza kuelekea mchezo huo kesho Allison amesema kwanza anajivunia kucheza fainali yake ya kwanza ya michuano ya FA tangu alipojiunga.

“Tunataka kubeba ubingwa wa FA, ni kitu ambacho kipo katika mipango yetu tangu msimu unaanza, tuna nafasi nzuri ya kushinda mchezo huu, tutacheza kwa kiwango kikubwa kila mtu amepania na hautakuwa mchezo rahisi kwa Chelsea,” amesema Allison.

Advertisement

Liverpool imebakiza michezo minne ya kucheza kabla ya msimu kuisha licha ya kupoteza matumaini ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya kutoka sare ya bao 1-1 ilipocheza dhidi ya Tottenham wiki iliyopita na kuipa nafasi Manchester City kutetea ubingwa wao kwa mara ya pili mfululizo.

Kwa upande wa Chelsea inaelekea kwenye fainali hiyo Wembley baada ya kuonyesha kiwango kibovu katika mechi zao tano za mwisho, vijana wa Thomas Tuchel wameshinda mchezo mmoja tu katika mechi hizo tano.

Advertisement