Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sita zampa jeuri Mkenya wa Mtibwa

CHIPO Pict

Muktasari:

  • Chipo aliyewahi kuzifundisha Pamba Jiji, Coastal Union na TRA United zamani Tabora United, amesema kikosi hicho kinatengeneza nafasi nyingi za kufunga, lakini umaliziaji umekuwa ni tatizo jambo analopambana nalo.

KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Yusuf Chipo raia wa Kenya, amesema mechi sita za Ligi Kuu Bara alizoiongoza timu hiyo hadi sasa zimempa mwangaza zaidi, ingawa moja ya jambo kubwa analopambana nalo ni kuongeza ufanisi katika eneo la ushambuliaji.

Chipo aliyewahi kuzifundisha Pamba Jiji, Coastal Union na TRA United zamani Tabora United, amesema kikosi hicho kinatengeneza nafasi nyingi za kufunga, lakini umaliziaji umekuwa ni tatizo jambo analopambana nalo.

“Mwelekeo wetu hadi sasa ni mzuri lakini tunahitaji kuongeza jitihada zaidi kwa sababu ushindani ni mkubwa na mechi pia ziko karibu, wengi wa wachezaji wetu hapa ni vijana, hivyo wanaendelea kujifunza siku baada ya siku,” amesema Chipo.

Kocha huyo aliyeachana na Murang’a SEAL ya kwao Kenya tangu Agosti 21, 2025, amesema wakati anaendelea kupambana na hali iliyopo katika eneo la ushambuliaji, jambo muhimu ni kuendelea kuhakikisha kikosi hicho hakidondoshi pointi kizembe.

Tangu Chipo ateuliwe ndani ya Mtibwa Sugar Novemba 17, 2025 kuwa kocha mkuu akisaidiana na Awadh Juma ‘Maniche’, ameiongoza timu hiyo katika mechi sita za Ligi Kuu Bara, ambapo kati ya hizo ameshinda tatu na sare tatu, hajapoteza, huku ikifunga mabao sita na kuruhusu matatu.

Timu hiyo iliyorejea Ligi Kuu Bara 2025-2026, baada ya kushuka 2023-2024, ilianza msimu huu kwa kufundishwa na Awadh Juma ‘Maniche’ aliyeipandisha, kisha akaletwa Chipo kutokana na Maniche kutokuwa na vigezo vinavyokidhi kuongoza benchi la ufundi akiwa kocha mkuu wa timu ya Ligi Kuu.

Mechi sita za Chipo ndani ya Mtibwa matokeo yake yapo hivi; KMC 0-0 Mtibwa, Mtibwa 2-1 TRA United, JKT Tanzania 0-0 Mtibwa, Simba 1-1 Mtibwa, Mtibwa 2-1 Mbeya City na Mtibwa 1-0 Pamba Jiji.