Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkenya asaka straika Mtibwa  Sugar

KONDO Pict

Muktasari:

  • Kocha huyo wa zamani wa Pamba Jiji, Coastal Union na TRA United zamani Tabora United, alijiunga rasmi na Mtibwa Novemba 17, 2025, akishirikiana na Kocha Msaidizi, Awadh Juma 'Maniche' na hadi sasa hajapoteza mechi yoyote ya Ligi Kuu.

WAKATI dirisha dogo la usajili likifunguliwa kuanzia Januari Mosi, 2026, Kocha wa Mtibwa Sugar, Mkenya Yusuf Chipo amepeleka ripoti yake kwa uongozi ili kuboresha kikosi hicho, huku sehemu kubwa anayotaka ni kuongezewa mshambuliaji.

Kocha huyo wa zamani wa Pamba Jiji, Coastal Union na TRA United zamani Tabora United, alijiunga rasmi na Mtibwa Novemba 17, 2025, akishirikiana na Kocha Msaidizi, Awadh Juma 'Maniche' na hadi sasa hajapoteza mechi yoyote ya Ligi Kuu.

Tangu ajiunge na timu hiyo, Chippo aliiongoza katika mechi tatu za Ligi Kuu na kati ya hizo alishinda moja tu na kutoka sare mbili, huku safu ya ushambuliaji ikifunga mabao mawili, jambo analoona eneo hilo linahitaji kuboreshwa.

"Wastani wetu wa kufunga siyo mzuri kwa sababu tunatengeneza sana nafasi ingawa, jambo nzuri ni kuona hatupotezi pia na sisi, nadhani ni sehemu tunayoihitaji kuiangalia dirisha dogo na tayari viongozi wanalijua hilo," amesema Chippo.

Chippo aliyejiunga na Mtibwa baada ya kuachana na Murang'a SEAL ya kwao Kenya tangu Agosti 21, 2025, amesema baada ya kurejea kuendelea na maandalizi Januari 5, 2026, atatumia kuangalia wachezaji wengine ambao hawajacheza kwa muda mrefu.

Mtibwa inaongozwa na mshambuliaji, Andrew Simchimba aliyejiunga na kikosi hicho kwa mkopo akitokea Singida Black Stars na amefunga bao moja tu la Ligi Kuu, katika ushindi wa timu hiyo wa 2-0, dhidi ya Fountain Gate, Septemba 28, 2025.

Simchimba msimu uliopita akiwa na kikosi cha Geita Gold, aliibuka mfungaji bora wa Ligi ya Championship baada ya kufunga mabao 18, sawa na nyota mwenzake wanaocheza wote Mtibwa, Raizin Hafidh, ingawa hadi sasa hajafunga bao lolote Ligi Kuu.