Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ruto awapongeza, awazawadia wanamichezo Kenya

RUTO Pict

Muktasari:

  • Katika hafla ya chakula cha mchana kilichofanyika Ikulu ya Nairobi wikiendi iliyopita, Ruto amesema wanamichezo wa Kenya, kuanzia wanariadha, wachezaji wa soka, rugby, mpira wa wavu na hata ngumi aliowataja kuwa mabalozi wakuu wa taifa na mfano wa mshikamano wa kitaifa.

RAIS wa Kenya, William Ruto amewapongeza na kuwapa zawadi za heshima wachezaji wa timu ya Harambee Stars iliyshiriki michuano ya CHAN 2024 na wanamichezo wengine akiwahakikishia mazingira bora zaidi kwa michezo nchini humo.

Katika hafla ya chakula cha mchana kilichofanyika Ikulu ya Nairobi wikiendi iliyopita, Ruto amesema wanamichezo wa Kenya, kuanzia wanariadha, wachezaji wa soka, rugby, mpira wa wavu na hata ngumi aliowataja kuwa mabalozi wakuu wa taifa na mfano wa mshikamano wa kitaifa.

Akirejelea safari ya Harambee Stars katika mashindano ya CHAN 2024 yaliyoandaliwa na nchi nchi hiyo ikishirikiana na Tanzania na Uganda, Rais amesisitiza matokeo ya timu hiyo yameonyesha 'Hakuna lisilowezekana Wakenya wakicheza kwa moyo, nidhamu na mshikamano.' Kenya iliibuka kinara wa Kundi A lililokuwa la kifo baada ya kuibwaga vigogo kama Morocco na DR Congo kisha kwenda kutolewa robo fainali na Madagascar ambao usiku wa jana walivaana na Morocco katika mechi ya fainali na kupoteza kwa mabao 3-2.

Rais alitumia jukwaa hilo pia kutangaza nyongeza kubwa ya zawadi kwa wanamichezo akiwema bayana kwamba mwanariadhaa atakayetwaa medali ya Dhahabu ya Olimpiki kwa sasa italipwa KSh 3 milioni (kutoka 750,000).

Atakayenyakua medali ya Fedha ni KSh 2 milioni na Shaba KSh 1 milioni.

Katika michezo ya timu, kila mchezaji wa dhahabu atapata KSh 750,000, fedha KSh 500,000, na shaba KSh 375,000.

Kwa jumla, zaidi ya KSh 70 milioni zimetengwa kwa malipo ya hivi karibuni na bonasi za kuvunja rekodi.

Mbali na zawadi, serikali imetangaza uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya michezo. Viwanja vya Kasarani, Nyayo, Eliud Kipchoge, Bukhungu na Raila Odinga vinakarabatiwa, huku Talanta Sports City ikiendelea kujengwa.

Aidha, zaidi ya Akademia 37 za michezo zimeanzishwa kwenye maeneo ya bunge mbalimbali nchini.

“Dira yetu ni kuifanya Kenya kuwa nguvu kubwa ya michezo barani Afrika na duniani, tukiweka macho yetu kwenye AFCON 2027 na mashindano makubwa zaidi,” amesema Rais Ruto na kuongeza kwa kuwahimiza wanamichezo kuendelea kuvunja rekodi, kuinua bendera ya Kenya juu na kuhamasisha mamilioni duniani kote.