Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha wa Rugby Ubelgiji afia mashindanoni Kenya

RUGBY Pict

Muktasari:

  • Kocha huyo mwenye umri wa miaka 43, mzaliwa wa Afrika Kusini, alizirai akiwa katika Uwanja wa Nyayo na akapatiwa huduma ya kwanza na wahudumu wa afya kabla ya kupelekwa hospitalini jijini Nairobi.

Kocha wa timu ya taifa ya wanawake ya Ubelgiji ya Rugby Sevens, Warren Abrahams, amefariki dunia wakati wa mashindano ya Safari Sevens yaliyofanyika jijini Nairobi, Kenya, siku ya Ijumaa Oktoba 10, 2025, kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Rugby la Kenya (KRU) iliyotolewa Jumapili Oktoba 12, 2025.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 43, mzaliwa wa Afrika Kusini, alizirai akiwa katika Uwanja wa Nyayo na akapatiwa huduma ya kwanza na wahudumu wa afya kabla ya kupelekwa hospitalini jijini Nairobi.

“KRU inaomboleza kifo cha ghafla cha Warren Abrahams, kocha wa timu ya taifa ya wanawake ya Ubelgiji waliokuwa nchini kushiriki mashindano ya Safari Sevens,” imesomeka sehemu ya taarifa ya KRU.

RUG 01

“Tunaungana na familia yake, marafiki na jamii nzima ya rugby ya Ubelgiji katika kipindi hiki kigumu,” taarifa hiyo imeongeza.

KRU imesema kuwa kocha huyo, ambaye pia aliwahi kuwa kocha mkuu wa timu ya Wales, atakumbukwa kwa shauku, weledi na kujituma kwake katika kukuza mchezo wa rugby.

Mwenyekiti wa KRU, Harriet Okach, amesema walichelewesha kutangaza taarifa ya kifo hicho hadi familia yake nchini Afrika Kusini ilipofahamishwa. Aidha, familia iliiomba taarifa hiyo isitangazwe hadharani hadi walipowasili Nairobi.

Timu ya Ubelgiji ilijiondoa kwenye mashindano hayo kufuatia kifo cha kocha wao, huku chanzo cha kifo chake kikielezwa bado hakijafahamika.

Katika taarifa yake, Shirikisho la Rugby la Ubelgiji limesema: “Rugby ya Ubelgiji ipo katika majonzi kufuatia kifo cha ghafla cha Warren Abrahams, kocha mkuu wa BelSevens.”

RUG 02

Shirikisho hilo limeongeza kuwa limechukua hatua zote muhimu kusaidia wachezaji na benchi la ufundi kupita katika kipindi hiki kigumu.

“Timu tayari imerejea Ubelgiji na itaendelea kupata usaidizi wa kisaikolojia ili kukabiliana na mshtuko huu,” taarifa hiyo imesema.

Mashindano ya Safari Sevens hufanyika kila mwaka nchini Kenya na hushirikisha timu za taifa na klabu kutoka mataifa mbalimbali duniani.