Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Elizabeth Muteshi aeleza hisia zake akiitwa mara ya kwanza kuichezea Harambee Starlets

MUTESHI Pict

Muktasari:

  • Kocha mkuu wa Starlets, Beldine Odemba, ametangaza kikosi cha wachezaji 38 kwa ajili ya mechi dhidi ya Gambia, ambayo itachezwa kwa mfumo wa nyumbani na ugenini.

Kiungo wa kati Elizabeth Muteshi, amesema kuitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha Harambee Starlets kumemfurahisha pamoja na kumpa ari mpya ya kupambana, huku Kenya ikijiandaa kwa mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026 dhidi ya Gambia, baadaye mwezi huu.

Kocha mkuu wa Starlets, Beldine Odemba, ametangaza kikosi cha wachezaji 38 kwa ajili ya mechi dhidi ya Gambia, ambayo itachezwa kwa mfumo wa nyumbani na ugenini.

Elizabeth amesema alikuwa akiamini kuna siku ataitwa kwenye kikosi cha Harambee Starlets, lakini hakujua ni lini, hivyo hatua ya kutajwa kwa jina lake miongoni mwa wachezaji wanaounda kikosi cha timu hiyo ameipokea kwa furaha sana.

MUTE 01

“Nilihisi furaha kubwa kuitwa kwenye kikosi cha Harambee Starlets, nilijua kuna siku ningeitwa, lakini sikufahamu ingekuwa lini,” amesema Elizabeth, ambaye aliwahi kuichezea Rising Starlets kwenye mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia la U20 mwaka 2023 dhidi ya Cameroon.

Hata hivyo, Elizabeth amefichua alichowahi kuambiwa na kocha wa kikosi cha U20, ambacho kilimpa morali ya kuendelea kupambana ili kufikia lengo la kuitwa kwenye timu ya Harambee Starlets.

“Kocha alituhimiza kufanya kazi kwa bidii na kulenga timu ya wakubwa, na tukifika huko, tuonyeshe uwezo wetu. Namshukuru Mungu kwa hatua hii. Nimepanga kufanya kazi kwa bidii zaidi ili nibaki kwenye timu ya wakubwa na kuiwakilisha nchi yangu,” amesema Elizabet. 

RATIBA YA MECHI
Mechi ya kwanza itapigwa Oktoba 24, 2025 kwenye Uwanja wa Nyayo, Nairobi nchini Kenya.
Mechi ya marudiano itachezwa Oktoba 28, 2025 kwenye Dimba la Lat Dior huko Thiès, Senegal.

MUTE 02
Kocha mkuu Harambee Starlets

WACHEZAJI WAPYA WALIOITWA
Kocha Odemba ameendelea kuchanganya wachezaji chipukizi na wale wenye uzoefu, kwa lengo la kujenga kikosi imara.

Kipa mpya: Mercy Akoth (Vihiga Queens)

Mabeki wapya: Dorcas Neema (Kibera Soccer Women), Lavyne Ochola (Kayole Starlet), Kikky Masika (Zetech Sparks), Lorine Ilavonga (aliyejiunga kutoka kikosi cha U20)

Viungo wapya: Elizabeth Muteshi, Keziah Ngaira (pia kutoka U20)

Washambuliaji wapya: Shirleen Opisa, Charity Midewa (wote kutoka Rising Starlets), Nicoline Hawa, mfungaji bora wa FKF (Ligi Kuu ya Wanawake 2024/25) kutoka Iron Ladies FC, pia ameitwa kwa mara ya kwanza.

“Tunajenga kikosi cha ushindani ambacho kina mchanganyiko wa wachezaji wenye uzoefu na vipaji vinavyochipukia. Hawa wachezaji wameonyesha njaa ya mafanikio, na sasa ni nafasi yao kuonyesha kuwa wanastahili kucheza kwenye timu hii,” amesema Odemba.

Tayari kikosi cha Harambee Starlets kimeshaingia kambini tangu Oktoba 5, 2025 kwa ajili ya maandalizi ya kuikabili Gambia.

Kenya imepanga kurejea katika mashindano ya Afrika, baada ya kushiriki kwa mara ya mwisho mwaka 2016.