Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Harambee Starlets kujipima ubavu na Algeria

Muktasari:

  • Starlets inarejea kwenye michuano hiyo baada ya kupita takribani miaka kumi, tangu ilipocheza kwa mara ya kwanza na ya pekee mwaka 2016.

KIKOSI cha Timu ya Taifa ya Soka Wanawake Kenya, Harambee Starlets, leo Novemba 25, 2025 kitashuka dimbani kumenyana na Algeria katika mechi ya kirafiki kama sehemu ya maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026 zitakazofanyika Morocco.

Starlets inarejea kwenye michuano hiyo baada ya kupita takribani miaka kumi, tangu ilipocheza kwa mara ya kwanza na ya pekee mwaka 2016.

Kocha Beldine Odemba anatumia mechi mbili za kirafiki dhidi ya Algeria kuchuja kikosi chake kuelekea mashindano hayo yatakayoanza Machi 17, 2026 hadi Aprili 3, 2026. Katika viwango vya dunia, Kenya inashika nafasi ya chini kwa tofauti ya nafasi 60 dhidi ya Algeria walioko nafasi ya 80 duniani.

Odemba aliita nyota wapya pamoja na waliorejea katika kikosi cha wachezaji 23, huku baadhi ya waliocheza dhidi ya Gambia ambapo Starlets ilishinda jumla ya mabao 4-1, wakikosa nafasi.

Wachezaji wapya na wale wa kawaida wanatarajiwa kupambana vilivyo ili kumvutia kocha na kujihakikishia namba kwenye kikosi cha mwisho.

Mechi hizi za kirafiki zitampa Odemba na benchi lake la ufundi nafasi ya kuwapima wachezaji kabla ya michuano mikubwa mwakani.

Golini, Lilian Awuor ana nafasi kubwa ya kuanza, ingawa Annedy Kundu aliyekuwa benchi kwenye mechi za kufuzu anaweza pia kupewa nafasi.

Katika safu ya ulinzi, beki wa Zetech Sparks, Sheryl Muyera, ataangaliwa kwa karibu katika majukumu yake ya kwanza ya timu ya taifa. Hata hivyo, atakutana na ushindani kutoka kwa wazoefu Ruth Ingotsi, Dorcas Shikobe, Enez Mango, Leah Andiema, Vivian Nasaka, pamoja na chipukizi Lorine Ilavonga wa Ulinzi Starlets.

Safu ya kiungo itawashuhudia Corazon Aquino akijaribu kurejesha nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza baada ya kuanzia benchi dhidi ya Gambia. Pia wapo nahodha wa Rising Starlets, Fasila Adhiambo, Elizabeth Muteshi, Martha Amunyolet, Medina Abubakar na Providence Mukalo.

Katika ushambuliaji, Odemba ana wachezaji wengi wenye uwezo. Mwanahalima Adam, Elizabeth Wambui na Shirleen Opisa wana nafasi kubwa ya kuanza. Wengine wanaowania namba ni Euphraiser Shilwatso, Valerie Nekesa, Emily Moranga na Airin Madalina.

Mechi dhidi ya Algeria inatarajiwa kumpa Odemba taswira sahihi ya kikosi kitakachopeperusha bendera ya Kenya katika WAFCON 2026 nchini Morocco.