Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gor Mahia yazinduka, Tusker yapasuka tena 

KPL Pict

Muktasari:

  • K'Ogalo iliyopoteza mechi ya ufunguzi ya KPL mbele ya Bidco Utd kwa kulala 1-0, lakini leo imewageuzia kibao Sofapaka kwa mabao  yaliyofungwa kila moja katika kipindi kupitia kwa Ebenezer Adukwa.

Mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu ya Kenya, Gor Mahia imezinduka jioni hii baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Sofapaka, huku Tusker ikipasuka kwa mara nyingine katika ligi hiyo.

K'Ogalo iliyopoteza mechi ya ufunguzi ya KPL mbele ya Bidco Utd kwa kulala 1-0, lakini leo imewageuzia kibao Sofapaka kwa mabao  yaliyofungwa kila moja katika kipindi kupitia kwa Ebenezer Adukwa.

Bao la kwanza lilifungwa dakika ya 32 na kudumu hadi mapumziko, huku Austin Odhiambo alikosa penalti dakika chache baada ya bao hilo la Ebenezer.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ya wachezaji, lakini ni K'Ogalo ilinufaika kwa kuweka chuma cha pili kupitia kwa  Ebenezer tena kwa shuti kali la mita 40 toka langoni mwa Sofapaka.

Ushindi huo umeifanya Gor Mahia kuvuna pointi tatu za kwanza msimu huu na kushika nafasi ya nne katika msimamo.

Katika mechi nyingine za mapema, Mara Sugar ilibanwa nyumbani na Kakamega Homeboyz kwa kutoka suluhu, huku Tusker ikikandikwa tena 2-1 na Rangers ikiwa ugenini baada ya wiki iliyopita kuanza na kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa KCB. Ushindi huo umeifanya Posta kuongoza msimamo kwa kufikisha pointi sita na mabao manne.

Huku kipigo hicho cha pili kwa  Tusker ambao ni  mabingwa wa zamani Kenya kushika mkia kwa sasa baada ya mechi za raundi ya pili kupigwa.

Jana Ijumaa ilishuhudiwa KCB ikichezea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Mathare United.