Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

David Ouma apata dili jipya Kenya

OUMA Pict

Muktasari:

  • Ouma alifanya kazi Mathare United akiwa kocha msaidizi kuanzia mwaka 2004 hadi 2005, kisha mwaka 2006 akateuliwa kuifundisha timu ya vijana hadi mwaka 2009. Sasa amerejea tena kwa mara ya tatu, lakini safari hii amejiunga nayo kama kocha mkuu.

ALIYEKUWA Kocha wa Singida Black Stars, David Ouma amejiunga na Klabu ya Mathare United ya kwao Kenya, huku akiweka wazi ni sehemu sahihi kwake kuendelea kuonyesha ubora wake, baada ya awali pia kuwahi kufanya kazi katika kikosi hicho.

Ouma alifanya kazi Mathare United akiwa kocha msaidizi kuanzia mwaka 2004 hadi 2005, kisha mwaka 2006 akateuliwa kuifundisha timu ya vijana hadi mwaka 2009. Sasa amerejea tena kwa mara ya tatu, lakini safari hii amejiunga nayo kama kocha mkuu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ouma amesema baada ya kuondoka Singida alipata ofa kutoka timu mbalimbali za kwao Kenya na nje ya mipaka ya nchi hiyo, lakini kutokana na uhusiano mzuri aliokuwa nao na Mathare United, ameamua kurejea kikosini.

OUM 01

“Baada ya kuondoka Singida nilihitaji muda zaidi wa kupumzika lakini uongozi wa Mathare United ulinifuata na kuniambia wanahitaji huduma yangu. Kiukweli ilikuwa ni vigumu kuwakatalia kutokana na ushirikiano wetu tulionao,” amesema Ouma.

Kocha huyo aliyeifundisha Singida kuanzia mwaka 2024 hadi 2026 aliachana nayo Aprili 5, 2026, ikiwa ni muda mfupi tangu ipoteze kwa mabao 2-0 dhidi ya TRA United katika mechi ya Ligi Kuu iliyopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Katika msimu wa 2025-2026, Ouma aliiongoza Singida katika mechi 17 za Ligi Kuu na alishinda saba, akatoka sare nne na kupoteza sita, akiiacha ikiwa nafasi ya sita na pointi 25, huku ikifunga mabao 19 na kuruhusu 19.

Ouma, ambaye pia aliwahi kuifundisha Coastal Union, anakumbukwa sana katika kikosi hicho cha ‘Wagosi wa Kaya’, kwani msimu wa 2023-2024 aliwezesha timu hiyo kumaliza nafasi ya nne katika Ligi Kuu Bara na kufuzu Kombe la Shirikisho Afrika.

Mafanikio hayo yaliifanya Coastal Union kufuzu michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza tangu iliposhiriki mara ya mwisho mwaka 1989 na kuishia raundi ya kwanza.

OUM 02

Ouma alijiunga na Coastal Union Novemba 9, 2023, akichukua nafasi ya aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi hicho na Mkurugenzi wa Programu za Vijana, Mwinyi Zahera, huku akiwa na uzoefu pia wa kuifundisha Sofapaka FC, Mathare United na Posta Rangers zote za kwao Kenya.

Kocha huyo mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 21 katika soka la Kenya ana leseni ya UEFA na CAF A, pamoja na uzoefu kutoka kituo cha michezo cha Ajax Amsterdam cha Uholanzi. Pia aliwahi kufundisha timu ya taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’ chini ya Bobby Williamson.

Mbali na hilo, Ouma anasifiwa kuiongoza timu ya taifa ya wanawake ya Kenya ‘Harambee Starlets’ kufuzu kwa mara ya kwanza Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON 2016).

Pia alikuwa na mafanikio makubwa akiwa na Sofapaka FC, akiisaidia kutwaa ubingwa wa ndani wa GOtv Shield mwaka 2014, kabla ya baadaye kuteuliwa kuhudumu kama mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo 2023.