Prime
Zile vurugu Simba, Berkane adhabu hii hapa

Muktasari:
- Katika mchezo huo Berkane ilitwaa ubingwa, kulikuwa na tukio lililosambaa sana katika mitandao ya kijamii likionyesha baadhi ya watu waliokuwa wamevalia jezi za Simba wakiwa katika chumba cha kubadilishia nguo cha waamuzi wakiwa wanarekodi video kwa kutumia simu yao.
MASHABIKI wa Simba bado wanaendelea kujiuliza kutokana na timu hiyo kupoteza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika mbele ya RS Berkane, Morocco lakini gumzo ni kile kilichotokea mara baada ya pambano hilo lililochezwa kwenye Uwanja wa New Amaan, visiwani Unguja.
Katika mchezo huo Berkane ilitwaa ubingwa, kulikuwa na tukio lililosambaa sana katika mitandao ya kijamii likionyesha baadhi ya watu waliokuwa wamevalia jezi za Simba wakiwa katika chumba cha kubadilishia nguo cha waamuzi wakiwa wanarekodi video kwa kutumia simu yao.
Kundi hilo la watu lilionekana kumrekodi mwamuzi wa mchezo huku wakijaribu kutupiana naye maneno, wakati huo refa wa mchezo naye na wasaidizi wake walikuwa wakichukua video ya tukio hilo.
Kutokana na tukio hili, shirikisho la soka barani Afrika huenda likatoa adhabu kwa wahusika ambapo kwa wa kanuni za Ukiukaji wa Maadili na Vitendo vya Fujo kifungu cha Kifungu cha 82 kinachoeleza kuhusu vitendo vya fujo, ikiwa ni pamoja na vurugu, vitisho, au vitendo vyovyote vinavyohatarisha usalama wa waamuzi, wachezaji, au mashabiki adhabu yake inawea kuwa faini au kufungiwa kushiriki shughuli za mpira wa miguu kwa kipindi maalumu ikitegemea na ukubwa wa tukio.
Vilevile kupitia kanuni hiyo pia kifungu cha 123, kinaeleza adhabu sawa za kupigwa faini au kufungiwa kujihusisha na masuala ya soka zinaweza kutolewa ikiwa mchezaji, kiongozi au shabiki atafanya vitendo vya fujo kiwanjani.
Baada ya tukio kutokea taratibu zinazofuatwa ni pamoja na uchunguzi wa tukio, uwasilishaji wa ushahidi, na uamuzi wa Kamati ya Nidhamu ya CAF. Mbali ya adhabu, mtu atakayekutwa na hatia pia anaweza kupewa onyo kali.