Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ZFF kutoa mafunzo ya kuwandaa wachezaji

ZFF Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ZFF na kusainiwa na Ofisa Habari wa Shirikisho hilo, Mohamed Hassan Kabwanga, kozi hiyo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uwezo wa makocha nchini katika masuala ya maandalizi ya kimwili kwa wachezaji.

SHIRIKISHO la Soka Zanzibar (ZFF) limetangaza kuanza kutoa kozi ya Utimamu wa Mwili Level 1 (Physical Fitness) kuanzia Juni 22 hadi 27, 2026.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ZFF na kusainiwa na Ofisa Habari wa Shirikisho hilo, Mohamed Hassan Kabwanga, kozi hiyo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uwezo wa makocha nchini katika masuala ya maandalizi ya kimwili kwa wachezaji.

Taarifa hiyo, imesema kozi hiyo inalenga kuwajengea makocha uelewa wa kitaalamu kuhusu mbinu za utimamu wa mwili, upangaji wa mazoezi na namna ya kuongeza uwezo wa wachezaji katika ushindani wa soka la kisasa.

MALI 02

Pia, katika taarifa hiyo ilitaka waombaji kujua kusoma na kuandika lugha ya Kiswahili na Kiingereza pamoja na kuwa na angalau cheti cha ukocha cha Diploma D ili waweze kushiriki mafunzo hayo.

"Washiriki wa kozi hiyo watatakiwa kulipa ada ya Sh500,000 itakayolipwa kupitia akaunti ya shirikisho," ilisema taarifa hiyo.

HABA 02

Sambamba na hayo, ilifafanua kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa kuendelea kukuza taaluma ya ukocha Zanzibar kwa kuwapa makocha maarifa ya kisasa yanayoendana na maendeleo ya mchezo wa soka duniani.

Aidha, makocha wenye sifa wametakiwa kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na kozi hiyo ambayo itasaidia kuongeza kiwango cha ushindani wa timu mbalimbali nchini.